3560; Njia nzuri ya kulipwa.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Fedha ni kiungo muhimu kwa maisha ya kila binadamu.

Na njia bora ya kupata fedha ni kutoa thamani kwa wengine.

Zipo njia nyingi za kutoa thamani kwa watu wengine.

Lakini njia bora zaidi ni ile ambayo kwako ni kama mchezo.

Njia hiyo inaanza kwa wewe kuwa halisi kwako.

Yaani unalipwa kwa kuwa wewe.

Kwa kufanya yale unayopenda, ambayo ndiyo uko imara zaidi.

Mara nyingi hutaweza kuanzia hapo, kwa sababu huenda unayopenda yanahitaji muda mpaka kuthaminiwa na wengine.

Hapo utalazimika kuanza na chochote kinachokuingizia fedha za kuendesha maisha.

Lakini hilo halipaswi kukusahaulisha kujijenga kwenye yale maeneo unayopenda ili uweze kuwa kwenye njia sahihi zaidi kwako.

Mafanikio makubwa yanataka mtu kutoa thamani kubwa na kwa muda mrefu bila kuacha.

Kuwa wewe, kwa kufanya unayopenda na ambayo una msukumo kutoka ndani yako hakuwezi kukuchosha.

Rafiki, je unayofanya sasa kukuingizia kipato ndiyo unayopenda zaidi au inakubidi tu kufanya?
Kama bado hujafika kwenye njia sahihi, anza kuijenga mapema ili uweze kutoa thamani kubwa inayohitajika kwa muda mrefu kwenye mafanikio.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe