3563; Kitu kibaya kuliko ujinga.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Ujinga ni kikwazo kikubwa cha mafanikio kwa walio wengi.

Watu wengi hawafanikiwi kwa sababu hawajui nini hasa wanachotaka.

Na hata wakijua wanachotaka, hawajui jinsi ya kukipata.

Lakini kuna kitu kingine kibaya kuliko ujinga, ambacho ni kujua nusu.

Hapa mtu anakuwa anajua, lakini kujua kwake hakujakamilika.

Kwa mtu kutumia kile anachojua kwa kiasi, kunapelekea kujikwamisha au kupata matokeo ambayo yanampoteza kabisa.

Watu wakisikia mafanikio yanataka mtu kuwa na njia nyingi za kuingiza kipato, wanakimbilia kuanza kufanya vitu vingi kwa pamoja.

Matokeo yake ni wanashindwa kufanikiwa kwenye hayo mengi wanayohangaika nayo.

Ni kweli waliofanikiwa wana vyanzo vingi vya kuingiza kipato, lakini siyo walipoanzia.

Walianza kwa kuweka umakini wao wote kwenye kitu kimoja mpaka kikasimama vizuri, kisha kwenda kwenye kitu kingine.

Kujua vitu nusu nusu ni sumu mbaya kuliko kutokujua kabisa.
Kwa sababu hicho unachokuwa unajua kwa kiasi kinakupoteza zaidi.

Rafiki, ni vitu vingapi unahangaika navyo sasa ambavyo vyote vinakutegemea moja kwa moja? Chagua kimoja utakachokipa umakini wako wote na kupumzisha vingine mpaka hicho kimoja kisimame imara.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe