3578; Usisingizie ushauri.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,

Kuna watu wamekuwa wanakwama kupata kile wanachotaka kwenye maisha na kusingizia kwamba wanakosa ushauri na miongozo sahihi.

Nasema hicho ni kisingizio kwa sababu siyo kitu halisi kinachoweza kumzuia mtu.

Ukiwa na njaa ya chakula, huhitaji ushauri wowote kuhusu kula, unataka chakula na utahakikisha unakipata.

Ukiwa na kiu ya maji huhitaji mwongozo wowote kuhusu kiu na maji. Unajua kwamba unakiu na unachotaka ni maji. Utapambana mpaka uyapate.

Halafu inakuja kwenye mafanikio na unasema hufanikiwi kwa sababu umekosa ushauri na miongozo?

Na unataka tukuamini, kweli?

Kama unataka kufanya makubwa, unatakiwa ufanye makubwa.
UFANYE.
Unaweza kushauriwa na kuongozwa utakavyo.
Lakini mwisho wa siku ni UMEFANYA?
Kama hujafanya, hayo mengine yote ni kujifurahisha tu.

Kama hujapata unachotaka, jiambie tu ukweli kwamba hujafanya unachopaswa kufanya.
Kama utajiambia kingine zaidi ya hicho, unajidanganya na utajizuia kupata mafanikio unayotaka.

Rafiki, ni mara ngapi umejiambia kama ungepata ushauri na mwongozo sahihi ungekuwa mbali?
Ni wakati sasa wa kujiambia ukweli, kwamba hujafanya yale unayopaswa kufanya.
Pambana na hayo na utaweza kupiga hatua unazotaka.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe