3585; Huenda pana ukweli.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa tunapenda kujifunza kwa wale ambao tunakubaliana nao.
Wale tusiokubaliana nao huwa tunaona hakuna tunachoweza kujifunza kwao.
Lakini hiyo ni njia ya kujifungia na kukosa fursa nzuri ya kujifunza.
Kuna kitu cha wewe kujifunza kwa kila mtu, hata kwa wale ambao hukubaliani nao kabisa.
Kwa sababu tu hukubaliani na watu, haimaanishi hawapo sahihi.
Huenda pana ukweli kwenye yale yanayoamini, pamoja na wewe kutokubaliana nayo.
Wajibu wako namba moja kwenye maisha ni kujifunza.
Na hupaswi kuwa na mipaka kwenye kujifunza, kwa kuchagua nani wa kujifunza kwake na nani siyo wa kujifunza.
Ukitaka kujifunza vitu vya tofauti, jilazimishe kuwaelewa wale ambao hukubaliani nao.
Angalia ni ukweli gani ambao wao wanajiona wanausimamia.
Tabia ya ukweli ni kuwa haujali hisia.
Ukweli unabaki kuwa ukweli, hata kama mtu hupendi kuhusu ukweli huo.
Wajibu wako ni kuweka hisia zako pembeni na kuangalia ukweli uko wapi.
Ukiuona ukweli popote, upokee na kuutumia, hata kama unatoka kwa mtu ambaye hukubaliani naye.
Rafiki, ni mara ngapi umekuja kugundua kulikuwa na ukweli kwa watu ambao hukuwa unakubaliana nao?
Kuanzia sasa, tambua kwamba ukweli haujali hisia. Jiweka kwenye ngazi ya kuujua ukweli bila kujali hisia zako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
+255 678 977 007 | http://www.amkamtanzania.com
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe