DARASA LA UWEKEZAJI; JINSI YA KUFIKIRI KWA USAHIHI KAMA MWEKEZAJI (NGUZO 5 ZA KUKUIMARISHA)
Rafiki,
Watu wengi wanasikia kuhusu uwekezaji na hupenda kujaribu kuwekeza. Lakini mara nyingi, wanapojaribu, hawadumu kwa muda mrefu. Wengi hudhani kinachowazuia ni ukosefu wa elimu – na ni kweli, elimu ina mchango mkubwa.
Lakini jambo kubwa zaidi linalowakwaza wengi ni FIKRA zao juu ya uwekezaji.
Huwezi kufanikiwa katika uwekezaji kwa kufikiri vile ulivyokuwa unafikiri siku zote. Kuna fikra za kipekee ambazo ni lazima uwe nazo kama unataka kunufaika na uwekezaji kwa namna ya kipekee.
Kwa bahati mbaya, fikra hizo hazifundishwi wazi kwa watu wengi.
Lakini wewe una bahati kubwa – leo unaweza kuzijua na kuanza kunufaika nazo.
🎯 Ni kupitia DARASA LA UWEKEZAJI linalofanyika ndani ya programu ya NGUVU YA BUKU.

Kwenye darasa hili la kipekee, utajifunza: FIKRA KUU 5 ZA KIUWEKEZAJI ambazo ndizo NGUZO IMARA zitakazokusaidia kufanikiwa kama mwekezaji.
Kama tayari upo kwenye programu ya NGUVU YA BUKU
Jiandae vizuri na subiri muda wa darasa – usikose!
Kama bado hujaingia kwenye programu hii ya kipekee –
🌟 Chukua hatua sasa.
Programu ya NGUVU YA BUKU imeundwa kusaidia watu kama wewe kwenye eneo muhimu sana la USIMAMIZI WA FEDHA BINAFSI.
✅ Haina gharama
✅ Inapatikana kwa watu wote
✅ Inahitaji tu wewe kuwa tayari kujifunza na kuchukua hatua
NAMNA YA KUJIUNGA:
Unachotakiwa kufanya ni kuwa na nakala ya kitabu cha NGUVU YA BUKU, na kisha:
📲 Tuma ujumbe wa maneno: “NATAKA NGUVU YA BUKU” kwenda namba 0756694090
“NATAKA NGUVU YA BUKU”
Utapata maelekezo yote ya kujiunga mara moja.
💥 Usikubali kuendelea kujikwamisha kifikra unapokuja kwenye masuala ya uwekezaji.
Karibu kwenye darasa hili muhimu – uwekezaji wako unaanzia kwenye fikra zako.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukutakia mafanikio,
Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE
NGUVU YA BUKU