Mpendwa Rafiki,

Biashara si ya watu wenye mtaji mkubwa, ni ya watu wenye moyo mgumu na akili inayojifunza kila siku.

Watu wengi huona wajasiriamali kama matajiri wanaochekea benki,

…lakini hawajui kuna siku unalala bila kuuza, kuna wakati unaficha machungu mbele ya wateja, na kuna siku unajiuliza:

Kwa nini nilianza hii kitu?

Lakini kumbuka:

Uliingia huku kwa sababu hukutaka kuishi maisha ya kuamshwa kila asubuhi kwa sauti ya boss.

Uliamua kujitengenezea nafasi yako, sasa jenga misuli ya kuvumilia, kujifunza, na kubadilika.

Biashara yako inaweza kuwa ndogo, lakini ndoto yako haina ukubwa wa genge lako.

Labda unauza chipsi, mitumba, au bidhaa online.

Wengine wanakucheka, wanakuita (machinga).

Unakataliwa na benki, kodi inakusumbua, wateja hawalipi kwa wakati na bado familia inakutegemea wewe.

Lakini kumbuka, kila mjasiriamali mkubwa alianza kwenye kona ya mtaa, jikoni kwake, au na bidhaa 5 tu za kujaribisha.

Kama unasubiri biashara iwe kubwa ndipo ujitume haitafika huko.

Wengine walikataa kazi za mshahara mkubwa ili waanzishe biashara leo wanajuta.

Lakini si kwa sababu walichagua biashara, ni kwa sababu walikata tamaa mapema, walikataa kujifunza, walishindwa kuvumilia changamoto.

Biashara haifanikiwi kwa bidhaa tu,

…inafanikiwa kwa tabia, nidhamu, na maarifa ya mmiliki wake.

Zifuatazo Ni Hatua 3 Rahisi Za Kuijenga Biashara Yako Leo

  1. Kuza Maarifa, Sio Bei Tu.

Soma kuhusu mauzo, matangazo, huduma kwa wateja. Tazama YouTube. Sikiliza podcast. Usibaki tu ukihesabu faida, jenga akili yako.

  1. Tengeneza Mfumo wa Mauzo, Si Kukimbizana Tu!

Panga promosheni, andika namba za wateja, toa ofa maalum, tumia mitandao ya kijamii.

Siku zote uwe na mpango, usiendeshe kwa hisia.

  1. Wekeza kwenye Huduma Bora, Si Bei ya Chini Tu.

Wateja hawarudi kwa sababu bidhaa ni rahisi, wanarudi kwa sababu walipewa thamani.

Jali mteja mmoja leo, atakuletea watano kesho.

Biashara yako inakua kama na wewe unakua. Ukiwa mvivu, nayo inasinyaa.

Leo andika kwenye daftari Lako.

Ni wazo gani jipya la kuuza unaweza kujaribu wiki hii?

Ni tabia gani inachelewesha biashara yako, uchelewaji? Kutojibu simu? Kukosa ratiba?

Ni bidhaa ipi unaweza kuiuza kwa njia mpya? (Labda WhatsApp, TikTok, au delivery)

Chukua hatua moja kila siku, wiki mbili mbele utaanza kuona tofauti.

Hadithi Halisi: Zaituni Wa Tabora, Mama Wa Maboga ALIYEJENGA GHOROFA.

Zaituni alikuwa mama wa watoto watano, mkoani Tabora.

Alianza kuuza maboga sokoni, kila siku alikuwa akipata elfu mbili, tatu..

Watu walimcheka, na kumuuliza Haya ni maisha gani mama?

Lakini Zaituni alikuwa na ndoto. Alitenga faida ya elfu tano kila wiki, akanunua pikipiki ya kusambazia.

Alichukua kozi fupi ya kukuza mauzo mara mbili kwenye biashara yake kwa fedha alizochuma kwa jasho.

Baada ya miaka mitano, alinunua kiwanja, leo ana duka la vyakula jumla, anamiliki nyumba ya kupangisha, na watoto wake wote wako shule nzuri.

Anapenda kusema:

Nilichouza ni maboga, lakini nilichojenga ni heshima yangu.

Na wewe je? Utaendelea kubeba toroli au kuendesha biashara kwa mazoea?

Au utaamua kuitendea biashara yako kwa heshima, maarifa, na uthubutu, kama biashara ya mabilioni?

Anyway kama upo serious na biashara yako,

Na bado hujapata mifumo itakayokusaidia kuiendesha biashara yako kisasa na itakayokupa uhuru,

…bila kukutegemea wewe mmiliki.

Basi ni kama bahati kwako kwani mifumo hii unaipata leo kwenye package hii inayoitwa KUZA MAUZO PACKAGE,

Badala ya Tshs 300,000 Nzima,

Leo unaipata mifumo hii miwili (2) kwa Tshs 99,000 TU!- kwa mwaka mzima.

Mwisho wa ofa hii ni mwisho wa mwezi Huu,

Kuiwahi ofa hii ingia hapa 👇

https://wa.link/vwvw17

Karibu.
0756694090.
Imeandikwa na Ramadhan Amir