Kakaa/Dadaa..


Hivi unajua kuna watu wanawacheka wajasiriamali wadogo?


Huku wakiwasema vibaya:…

‎Mbona kila biashara unayoanzisha haifiki miezi mitatu?*


‎*Unapenda kulalamika sana!”


*Wewe huwezi fanikiwa kamwe!*


‎Na huwa naumia nikisikia haya maneno.
Kwa sababu…


Watu hawajui mateso yanayomfanya mtu aamue kuuza maandazi saa 12 asubuhi bila hata chai.


Hawajui…

‎Maumivu ya kutafuta mtaji wa elfu 20 kwa kuazima mia mia.

Kunyanyaswa na maneno ya jamaa zako:

‎‎ “Kama ni biashara ya maandazi si kila mtu anafanya?”

‎Kukesha ukitengeneza sabuni halafu asubuhi mvua inanyesha, hakuna mtu hata mmoja kununua.

Sasa leo nakuambia ukweli:

‎Siyo Kosa LAKO.

‎Haujafundishwa TU!..

‎Tatizo Si Wewe, Ni Mfumo Wetu.

‎Shule zetu hazikufundisha namna ya kuuza.

‎Hazikufundisha namna ya kujua faida.

‎Hazikufundisha namna ya kumshawishi mteja.

‎Tulifundishwa 1+1=2.

‎Lakini hatukufundishwa jinsi ya kutengeneza buku kwa kuuza karanga.

‎Ukatoka shule ukiwa na degree.

‎Au ukiwa form four au kidato cha 6.

‎Au hata bila cheti.

‎‎Lakini wote mko sokoni mnaanza biashara kama vipofu wanaovuka barabara.

‎Na Ndio Maana…

‎Unajikuta unafungua duka la vocha,

‎Unaanza kuuza na sabuni tano, pipi za mchina, na airtime ya mia.

‎Mwishoni mwa mwezi…
Umeuza elfu 50.
Umebakiwa na 10.

‎Na hata hujui imepotelea wapi.
Wewe si mzembe.
Wewe si mjinga.

‎Wewe ni mtu jasiri lakini hujapewa silaha.

‎Sasa Sikiliza Hii:

‎Kabla hujaanza biashara yoyote…

Unahitaji kujua vitu vitano tu vya msingi:

‎1. Shida ya watu ni ipi?
Watu hawataki bidhaa, wanataka suluhisho.

‎2. Unawauzia kina nani?
Hakuna biashara ya “kila mtu”


3. Unawafikiaje?
Kama hawaitwi hawaji. Kama hawajui hawanunui.

‎4. Bei yako inasemaje?
Bei nzuri haimaanishi rahisi inamaanisha INAOANA na thamani.

‎5. Faida yako iko wapi?
Si pesa inayoingia, ni pesa inayobaki baada ya gharama.

‎Stori Ya Kweli Ya Dada Zawadi Wa Gongo La Mboto….

‎Zawadi alikuwa anafua nguo kwa watu.

‎Kila siku jua likitoka, anajitwika ndoo, anazunguka mtaani akitafuta wateja wa kuwafulia hadi jioni.

‎Analipwa elfu mbili elfu tatu.
Anaondoka na macho mekundu, amechafuka huku mikono ikiwa imechubuka,


Lakini hana hela hata ya sabuni.
Siku moja alihudhuria semina ya biashara.

‎Akaambiwa kitu kimoja tu:
*Fungua huduma yako. Uisajili.

Toa package. Weka namba zako mitandaoni.*

‎Leo Zawadi haendi nyumba hadi nyumba.
‎Anapokea simu.
Wateja wanamfuata.

‎Anatoza elfu kumi hadi elfu ishirini kwa huduma ya kitaalamu.
Na bado anafua nguo.

‎Lakini kwa akili.
Tunaambiwa tukomae. Lakini hatuambiwi namna.

‎Tunaambiwa tufanye kazi kwa bidii. Lakini bidii bila maarifa ni kama kukata mti kwa kijiko.

‎SULUHISHO?
Sihitaji nikuambie uache biashara.

‎La hasha.
Nakuheshimu.
Ninachokuambia ni hivi:

‎Chukua hatua ya kutafuta elimu ya msingi ya biashara.

‎Elimu inayoeleweka.
Elimu ya mtaani.
Elimu ya kweli.

Kabla hujapoteza muda tena,
Kabla hujakataliwa tena,
Kabla hujachoka kujaribu jifunze.

‎Kwa Nini?

Kwa sababu:

‎Huwezi kufanikiwa kwa kukurupuka.
Na
Siyo kosa lako kuwa hujui.

‎Lakini litakuwa kosa lako ukikataa kujua.

‎Kama makala hii imekuongelea wewe, huna haja ya kujionea aibu.

‎Kila shujaa alianza akiwa hajui.
Lakini waliamua KUJIFUNZA.

‎Nataka nikupe silaha mbili.
Ni silaha za kuutokomeza ujinga,

‎Silaha hizo ni Elimu Ya Msingi Ya Biashara na CHUO CHA MAUZO, Kwa Mtu Wa Mtaa.

Zina mafundisho matupu, lugha nyepesi, na njia za kweli za kukuza biashara yako.

‎Unataka?

‎Kama unataka kupata silaha hizi mbili (2),

‎Bonyeza hapa 👇
*https://wa.link/38w2s1*


Karibu.
0756694090.
Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.


‎#SioKosaLako

‎#JifunzeUinuke

‎#BiasharaNiAkiliNaMaarifa