
Kama Unasubiri Bahati Umeshafeli Kabla Hujaanza!…
Rafiki Yangu,
Watu wengi wanaamini bahati ndiyo kila kitu.
Wanasema, Nikibahatisha tu dili moja kubwa, maisha yatabadilika.
Lakini ukweli mchungu ni huu,
ukikaa kungoja bahati, utakaa sana.
Wale wanaofanikiwa hawangoji upepo uende upande wao,
wanauumba upepo wao wenyewe.
Hawangoji nafasi, wanaitengeneza.
Kila siku unakutana na watu wanasema,
Maisha magumu bwana, sina bahati kama fulani.
Lakini ukichunguza kwa ndani,
wanaotajwa kuwa wenye bahatini watu wanaochukua hatua kila siku.
Wamejifunza kujiamini hata mambo yanapokuwa magumu.
Hawaogopi kuanza, hawaogopi kukosea.
Kwao kushindwa ni somo, sio hukumu.
Unajua kinachouma?
Ni kuona mtu mnaanza pamoja,
lakini baada ya miaka michache, yeye amepiga hatua kubwa,
na wewe bado uko pale pale.
Unaanza kujiambia, Labda yeye alibahatika.
Lakini ukweli unauma hakubahatika, aliamua.
Aliamua kufanya kitu leo,
wakati wengine wanasubiri hali iwe shwari.
Tatizo si ukosefu wa bahati,
tatizo ni kungoja mazingira yakamilike kabla ya kuanza.
Wakati wewe unasubiri kesho,
wenzako wanaijenga leo.
Bahati sio mpango.
Bahati ni matokeo ya maandalizi.
Na kama hujajiandaa, hata fursa ikipita mbele yako hautaiona.
Watu wanaofanikiwa wana mfumo.
Wamejenga falsafa ya maisha.
Wanajua wanataka nini,
wanajua kwanini wanakitaka,
na wanafanya kila siku hatua ndogo kuelekea huko.
Hawategemei maombi bila matendo.
Hawategemei kuombewa, wanajiombea kwa vitendo.
Kama unataka maisha yako yabadilike,
anza kubadili falsafa yako ya maisha.
Usiishi kwa mtazamo wa Nitangoja nione kama itaniendea vizuri.
Anza kufikiri kama mtu anayesababisha mabadiliko, sio anayesubiri mabadiliko.
Mafanikio hayaji kwa bahati,
yanakuja kwa maamuzi, kwa kujifunza, na kwa uvumilivu.
Kila siku unafanya maamuzi madogo,
na hayo ndiyo yanayojenga maisha yako makubwa kesho.
Watu wanaofanikiwa hawana miujiza,
wana mpangilio, nidhamu na mtazamo wa mafanikio.
Namkumbuka kijana mmoja kutoka Arusha.
Alikuwa akiuza chips kandokando ya barabara.
Wenzake walimcheka na wakimwambia hana bahati.
Lakini akaanza kujifunza kuhusu biashara, akasoma vitabu, akapanga malengo yake.
Baada ya miaka mitano,
yule asiye na bahati alikuwa anamiliki mgahawa wake,
ameajiri vijana watano,
na bado anasoma vitabu kila wiki.
Nilimuuliza, Uliwezaje?
Akacheka kidogo akasema,
Niliacha kusubiri bahati, nikaamua kuwa bahati mwenyewe.
Sasa hebu nikuulize wewe,
utangoja hadi lini?
Maisha yako hayataanza kubadilika mpaka uamue kuyabadili.
Bahati ni hadithi tuliyojiambia ili kujifariji.
Lakini mafanikio ni sayansi kuna kanuni, kuna mfumo, kuna falsafa.
Na ukitaka kuijua vizuri,
soma kitabu kipya cha FALSAFA YA MAISHA YA MAFANIKIO.
Kitabu hiki kitakufundisha jinsi ya kufanikiwa bila kutegemea bahati,
na jinsi ya kuunda mfumo wa maisha unaokuletea matokeo halisi.
Usisubiri bahati tengeneza bahati yako.
Anyway kama bado hujapata kitabu hiki,
Basi unaweza kubonyeza hapa 👇
Karibu.
0756694090.