
Rafiki Yangu,
Watu wengi wanahofia kutoa.
Wanaona kutoa kama kupoteza.
Wanasema, *Nikitoa, nitaishije?*
Lakini ukweli ni huu ustoa ni uwekezaji, si hasara.
Kila unachotoa, kinaacha alama,na kinakurudia kwa namna ambayo hujawahi kufikiria.
Tatizo kubwa la watu wengi ni hofu.
Hofu ya kupungukiwa, hofu ya kudharauliwa, hofu ya kujisahau.
Lakini kinachoshangaza ni hiki wale wanaotoa zaidi, ndio wanaopokea zaidi.
Toa muda wako kusaidia mtu,utagundua unapata heshima na fursa mpya.
Toa elimu, maarifa, tabasamu, au msaada,utashangaa jinsi maisha yanavyokulipa kwa njia tofauti.
Ustoa sio kutoa pesa tu.
Ni moyo wa kusema, *Nitachangia chochote nilichonacho, hata kidogo.*
Lakini leo hii, tumejenga jamii ya *nipeni, nipeni.*
Kila mtu anataka apokee, lakini wachache wako tayari kutoa.
Matokeo yake?
Tunaishi kwenye dunia yenye wivu, mashindano, na upweke.
Kila mtu anahisi anatumiwa.
Lakini ukweli ni kwamba, usipotoa moyo wako unakauka.
Unapoteza furaha, hamasa, na nguvu ya ndani.Kutoa ni tiba.
Ni kama kupumua huwezi kuvuta pumzi mpya kama hujaachia ya zamani.
Wengine wanasema, *Sina cha kutoa.*
Lakini huo ni uongo unaojificha kama ukweli.
Kila mtu ana kitu cha kutoa.
Mwingine ana muda, mwingine ana tabasamu, mwingine ana maneno ya faraja.
Kutoa sio kwa matajiri tu.
Ni kwa yeyote aliye hai na mwenye moyo.
Wanaosema ustoa ni hasara hawajui siri ya maisha, kuwa kila kitu kinachozunguka, hurudi.
Ustoa ni kama mbegu.
Hutegemei izae leo leo,…lakini unajua italeta mavuno siku moja, kwa namna isiyo ya kawaida.
Ustoa ni falsafa.
Ni mfumo wa kuishi unaokufanya usikose chochote.
Unapotoa kwa moyo safi, unaondoa hofu ya ukosefu.
Unafungua njia mpya zisizoonekana.Wale wanaotoa wanaishi kwa furaha.
Wanapata marafiki zaidi, wanapata fursa zaidi, Na wanaona maisha kwa jicho la matumaini.
Hauwi Mstoa kwa sababu ya kile ulichonacho, Unakua kwa sababu ya moyo ulionao.
Kutoa hakupunguzi kunaongeza. Kuna mama mmoja niliwahi kumfahamu, aliishi maisha ya kawaida sana.
Alikuwa anauza maandazi mtaani.
Lakini kila siku alikumbuka kutoa bakuli moja la maandazi kwa watoto wa jirani.
Watu walimcheka *Wewe unatoa wakati huna kitu?*
Miaka michache baadaye,mtoto mmoja wa yule jirani alifaulu vizuri, akapata kazi nzuri,na siku moja akarudi kumtafuta mama yule huku akisema,“Nikiulizwa nani aliyegusa maisha yangu, nakutaja wewe.
Ulinipa chakula wakati wengine walinipita.”Na tangu siku hiyo, maisha ya yule mama yakabadilika,akawa anapata msaada, fursa, na upendo kutoka kila pande.
Huo ndio ustoa urudi kusikotegemea.
Sasa jiulize,je, unatoa au unasubiri kuwa na vingi ndo uanze?
Maisha hayaanzi unapopokea,yanaanza unapotoa.
Kila kitu kizuri unachokitoa kinafungua mlango mpya.
Toa leo upate kesho usiyoitegemea.Na kama unataka kuelewa falsafa hii kwa undani zaidi,soma kitabu kipya: FALSAFA YA USTOA.
Kitakufundisha kwa nini kutoa ni nguvu,na jinsi ustoa unavyogeuka kuwa uwekezaji unaorudi kwa njia zisizo za kawaida.
Anyway, Kama bado hujakisoma unaweza kuanzia hapa 👇
Karibu.
0756694090.