
Rafiki Yangu,
Kuna kitu cha ajabu mno kinatokea ndani ya kila binadamu
Watu wanahangaika, wanakimbia kila kona, wanatafuta msaada, wanatafuta bahati, wanatafuta maombi, wanatafuta connection, wanatafuta mtu wa kuwainua…
…lakini bado maisha yao yapo pale pale.
Wanaishia kujiuliza,
Mbona kila mahali ninapogusa hakufunguki?
Mbona wengine wanapiga hatua fasta, mimi bado niko pale pale?
Au mimi nimezaliwa bila uwezo?
Lakini ukweli haujawahi kubadilika…
ustawi wa mtu hauji kutokea nje,
unatoka ndani.
Hujengewi unachomolewa kutoka ndani yako mwenyewe.
Ila tatizo kubwa ni hili…
Watu wengi hawajawahi kujitambua, kujisoma, au kujiwekea utaratibu wa ndani.
Wanatembea na hazina,
lakini hawajui namna ya kuifungua.
Kama simu imejaa apps nzuri,
lakini huna password,
hautafanya chochote nayo.
Hiyo ndiyo hali ya wengi wana uwezo,
lakini hawajaufikia kwa sababu haufunguki kwa nje, unafunguliwa kutoka ndani.
Sasa hapa ndipo maumivu yanazaliwa.
Unajiona unakwama,
na kuanza kuamini labda kuna kitu kinakuwekea vizuizi.
Unaona wengine wanafanikiwa haraka,
unaamini labda wao ndio walichaguliwa.
Unajisemea,
Labda mimi siyo mtu wa mafanikio.
Labda bado muda wangu.
Labda Mungu hajanitazama.
Lakini ukweli unaouma,
ni kwamba haujaanza safari ya kujifungua kwa ndani.
Tatizo si dunia,
tatizo si watu,
tatizo si bahati,
tatizo ni mlango wa ndani haujafunguliwa …na hiyo funguo ipo mikononi mwako.
Na ndio maana unaweza kusikia mawaidha,
kusoma vitabu,
kuhudhuria semina,
kuomba usiku kucha,
lakini maisha yakabaki vile vile.
Si kwamba hakuna nguvu,
ila hakuna ufunguo wa ndani uliotumika.
Hakuna mtu aliyekuja duniani akiwa maskini kiakili,
hakuna aliyezaliwa duni,
hakuna aliyeumbwa bila nafasi.
Lakini kuna tofauti mbili:
Kuna wanaotafuta nje, na kuna wanaochimba ndani.
Wale wanaotafuta nje huhangaika.
Wale wanaochimba ndani huendelea,
hata kama hawana kitu mwanzo.
Kwamba hutapata ustawi kwa kutegemea msaada,
kwa kuomba kila wakati bila kuchukua hatua,
…kwa kutafuta mtu wa kukuinua kila siku,
hiyo ni mindset iliyokosewa.
Ukweli ni huu:
Ustawi ni uwezo uliojengwa ndani yako kwa uelewa, nidhamu, na mabadiliko ya tabia sio msaada wa nje.
Suluhisho halipo mbali.
Halihitaji safari.
Halihitaji cheti.
Halihitaji uungwe mkono kwanza.
Halihitaji ukubalike.
Halihitaji kuonekana.
Linahitaji uamuzi mmoja tu…
Naamua kujiendesha kutoka ndani.
Hapo ndipo…
Unabadilisha namna unavyofikiri
Unajenga nidhamu mpya
Unaweka malengo yanayotekelezeka
Unajifunza kutawala tamaa
Unajua nini cha kukubali, nini cha kuacha
Unatengeneza mfumo, sio matamanio
Ustawi hauwaki kwa miujiza,
unawaka kwa ufahamu na maamuzi ya kila siku.
Ni mchakato wa ndani inayojengwa kimyakimya,
lakini matokeo yake yanaonekana nje hadharani.
Kuna jamaa mmoja nilimfahamu,
alikuwa na malalamiko kila siku.
Alikuwa anasema,
Bahati yangu bado haijafika.
Alikuwa anaanza miradi mingi,
lakini hakuna iliyoishi miezi miwili.
Si kwa sababu alikuwa hafai,
hapana.
Alikuwa hana mfumo wa ndani.
Siku moja nikamwambia,
Bro, acha kunung’unika. Jijenge ndani kwanza, usipange mafanikio yako kwa kelele, panga tabia zako kimya kimya.
Baada ya miezi kadhaa,
hakuwa yule wa zamani.
Hakuongea sana,
hakujitangaza,
lakini mfumo wake wa ndani ulianza kunukia.
Mapato yakabadilika.
Mahusiano yakatulia.
Maono yake yakapanuka.
Leo ananiambia,
Nimegundua siku zote nilikuwa na uwezo, nilikosa ufunguo tu.
Ustawi wako hauko mjini.
Hauko kwa watu.
Hauko kwa bahati.
Uko ndani yako.
Na unapochimba,
unauona.
Kujifunza zaidi soma kitabu kipya cha
FALSAFA YA USTOA – Jitawale Mwenyewe, Uitawale Dunia.
Kwa sababu mafanikio hayafunguki kwa dua tu,
yanachomolewa na ufahamu wa ndani.
Kukipata anzia hapa 👇
https://wa.link/524kl0
Karibu.
0756694090.