‎
‎Rafiki Yangu,
‎
‎Kuna kitu cha ajabu mno kinatokea ndani ya kila binadamu
‎
‎Watu wanahangaika, wanakimbia kila kona, wanatafuta msaada, wanatafuta bahati, wanatafuta maombi, wanatafuta connection, wanatafuta mtu wa kuwainua…
‎
‎…lakini bado maisha yao yapo pale pale.
‎
‎Wanaishia kujiuliza,
‎Mbona kila mahali ninapogusa hakufunguki?
‎
‎Mbona wengine wanapiga hatua fasta, mimi bado niko pale pale?
‎
‎Au mimi nimezaliwa bila uwezo?
‎
‎Lakini ukweli haujawahi kubadilika…
‎ustawi wa mtu hauji kutokea nje,
‎unatoka ndani.
‎
‎Hujengewi unachomolewa kutoka ndani yako mwenyewe.
‎
‎Ila tatizo kubwa ni hili…
‎Watu wengi hawajawahi kujitambua, kujisoma, au kujiwekea utaratibu wa ndani.
‎
‎Wanatembea na hazina,
‎lakini hawajui namna ya kuifungua.
‎
‎Kama simu imejaa apps nzuri,
‎lakini huna password,
‎hautafanya chochote nayo.
‎
‎Hiyo ndiyo hali ya wengi wana uwezo,
‎lakini hawajaufikia kwa sababu haufunguki kwa nje, unafunguliwa kutoka ndani.
‎
‎Sasa hapa ndipo maumivu yanazaliwa.
‎Unajiona unakwama,
‎na kuanza kuamini labda kuna kitu kinakuwekea vizuizi.
‎
‎Unaona wengine wanafanikiwa haraka,
‎unaamini labda wao ndio walichaguliwa.
‎
‎Unajisemea,
‎Labda mimi siyo mtu wa mafanikio.
‎Labda bado muda wangu.
‎Labda Mungu hajanitazama.
‎
‎Lakini ukweli unaouma,
‎ni kwamba haujaanza safari ya kujifungua kwa ndani.
‎
‎Tatizo si dunia,
‎tatizo si watu,
‎tatizo si bahati,
‎tatizo ni mlango wa ndani haujafunguliwa …na hiyo funguo ipo mikononi mwako.
‎
‎Na ndio maana unaweza kusikia mawaidha,
‎kusoma vitabu,
‎kuhudhuria semina,
‎kuomba usiku kucha,
‎lakini maisha yakabaki vile vile.
‎
‎Si kwamba hakuna nguvu,
‎ila hakuna ufunguo wa ndani uliotumika.
‎
‎Hakuna mtu aliyekuja duniani akiwa maskini kiakili,
‎hakuna aliyezaliwa duni,
‎hakuna aliyeumbwa bila nafasi.
‎
‎Lakini kuna tofauti mbili:
‎Kuna wanaotafuta nje, na kuna wanaochimba ndani.
‎
‎Wale wanaotafuta nje huhangaika.
‎Wale wanaochimba ndani huendelea,
‎hata kama hawana kitu mwanzo.
‎
‎Kwamba hutapata ustawi kwa kutegemea msaada,
‎kwa kuomba kila wakati bila kuchukua hatua,
‎…kwa kutafuta mtu wa kukuinua kila siku,
‎hiyo ni mindset iliyokosewa.
‎
‎Ukweli ni huu:
‎Ustawi ni uwezo uliojengwa ndani yako kwa uelewa, nidhamu, na mabadiliko ya tabia sio msaada wa nje.
‎
‎Suluhisho halipo mbali.
‎Halihitaji safari.
‎Halihitaji cheti.
‎Halihitaji uungwe mkono kwanza.
‎Halihitaji ukubalike.
‎Halihitaji kuonekana.
‎
‎Linahitaji uamuzi mmoja tu…
‎Naamua kujiendesha kutoka ndani.
‎
‎Hapo ndipo…
‎
‎Unabadilisha namna unavyofikiri
‎
‎Unajenga nidhamu mpya
‎
‎Unaweka malengo yanayotekelezeka
‎
‎Unajifunza kutawala tamaa
‎
‎Unajua nini cha kukubali, nini cha kuacha
‎
‎Unatengeneza mfumo, sio matamanio
‎
‎
‎Ustawi hauwaki kwa miujiza,
‎unawaka kwa ufahamu na maamuzi ya kila siku.
‎
‎Ni mchakato wa ndani inayojengwa kimyakimya,
‎lakini matokeo yake yanaonekana nje hadharani.
‎
‎Kuna jamaa mmoja nilimfahamu,
‎alikuwa na malalamiko kila siku.
‎Alikuwa anasema,
‎Bahati yangu bado haijafika.
‎
‎Alikuwa anaanza miradi mingi,
‎lakini hakuna iliyoishi miezi miwili.
‎Si kwa sababu alikuwa hafai,
‎hapana.
‎
‎Alikuwa hana mfumo wa ndani.
‎
‎Siku moja nikamwambia,
‎Bro, acha kunung’unika. ‎Jijenge ndani kwanza, ‎usipange mafanikio yako kwa kelele, ‎panga tabia zako kimya kimya.
‎
‎Baada ya miezi kadhaa,
‎hakuwa yule wa zamani.
‎Hakuongea sana,
‎hakujitangaza,
‎lakini mfumo wake wa ndani ulianza kunukia.
‎
‎Mapato yakabadilika.
‎Mahusiano yakatulia.
‎Maono yake yakapanuka.
‎
‎Leo ananiambia,
‎Nimegundua siku zote nilikuwa na uwezo, ‎nilikosa ufunguo tu.
‎
‎Ustawi wako hauko mjini.
‎Hauko kwa watu.
‎Hauko kwa bahati.
‎Uko ndani yako.
‎Na unapochimba,
‎unauona.
‎
‎Kujifunza zaidi soma kitabu kipya cha
‎FALSAFA YA USTOA – Jitawale Mwenyewe, Uitawale Dunia.
‎
‎Kwa sababu mafanikio hayafunguki kwa dua tu,
‎yanachomolewa na ufahamu wa ndani.
‎
‎Kukipata anzia hapa 👇
‎
‎https://wa.link/524kl0
‎
‎Karibu.
‎0756694090.
‎