Tunajua kwamba hakuna binadamu anayeweza kuishi milele, kwamba kila mtu baada ya muda fulani wa kuishi atakufa. Ambacho wengi hatujui ni kwamba sio kila tunaemzika anakuwa amekufa. Hapa simaanishi kwamba anakuwa amechukuliwa msukule na tunazika kivuli chake kama baadhi ya watu wanavyoamini, hapana. Namaanisha kuna watu ambao tunaendelea kuishi nao ama wanaishi kwenye maisha yetu hata baada ya kufa. Hivyo hatuwezi kusema watu hawa wamekufa bali tunasema wamepumzika.

  Kama unataka na wewe uendelee kuishi hata baada ya kufa basi jifunze kitu kutka hapa. Watu ambao wamekuwa na mchang mkubwa kwenye maisha ya watu, wamewasaidia watu kufikia lengo fulani ama wameweza kubadili maisha ya watu kuwa bora zaidi huwa wanakumbukwa milele. Watu hao wak kwenye makundi yafuatayo, vingozi, wanasayansi, wanaharakati, wagunduzi na hata watu walioweza kuzibadili familia zao.

  Viongozi walioleta ukombozi kwenye nchi zao au waliokuwa na uongozi wa kutukuka bado tunaishi na mpaka leo. wapo wengi ila wachache ni kama J.K Nyerere, Kwame Nkuruma, Jomo Kenyata, na Patrice Lumumba. Hawa mpaka leo tunaishi nao na kwa lolote tunalotaka kufanya lazima tuangalie kwanza kama wangekuwepo wangesemaje?

  Katika hayo makundi mengine kuna wanasayansi kama Albert Einstein, Isaac Newton, Michael Faraday, Marie Currie, Gregory Mendel na wengine wengi. Maendeleo makubwa ya kisayansi tunayoyafaidi leo yametokana na misingi iliyowekwa na watu hawa. Kwa upande wa wanaharakati tunao wakina Bibi Titi Mohamed, Oscar Kambona, Martin Luther King Jr, Malcom X. Hao ni baadhi tu ya wanaharakati ambao walipigania mambo mbalimbali enzi zao. Pia kuna watu ambao wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye familia zao, wanaleta mabadiliko makubwa na mazuri kiasi kwamba hata wanapokufa vizazi vya familia ama ukoo vinavyofuata vinaendelea kumkumbuka.

  Je na wewe unataka kuishi milele? Hujachelewa amua kufanya jambo ambalo litafanya maisha ya watu wanaokuzunguka kuwa bora zaidi. Kila mtu ana uwezo wa kipekee ambao akiutumia anaweza kuyanufaisha sana maisha ya wanaomzunguka na hata dunia nzima. Sisemi uanze kufikiria jinsi ya kugundua mambo ya kisayansi, hapana ila kama unaweza ni vizuri pia. Angalia jamii inayokuzunguka, inasumbuliwa na nini, ni tatiz gani hasa linafanya watu waone maisha ni magumu kwao. Kisha fikiria njia inayoweza kuwarahisishia maisha, kama utapata suluhisho bora basi litasambaa hata kufikia nchi nzima na hata dunia. Kama tatizo ni uongozi mbovu jipange kupata uongozi na kuwa na mpang madhubuti wa kusaidia watu. Kuna mambo mengi sana ambayo bado hayajafanywa ambayo yakifanywa yatarahisisha sana maisha ama yatapunguza ukali wa maisha. Ukomo ni fikra zako tu.