Kama unafikiri unaweza au kama unafikiri huwezi uko sahihi kabisa na wala hakuna anaeweza kukupinga. Kila kitu kinaanza na wewe mwenyewe. Akili yako na mawazo yako ndivyo vinavyotawala maisha yako. Binadamu ni matokeo ya yale anayoyafikiri kwa muda mrefu. Hivyo kama wewe unafikiri unaweza kufanya jambo ulilopanga, hakuna cha kukuzuia kulifanya. Hata kuwe na ugumu gani utatafuta njia yoyote ya kuweza kulifanya kwa sababu huo ndio uamuzi wako. Kama unafikiri huwezi kufanya jambo fulani hakuna anaeweza kukulazimisha kulifanya, hata ukishikiwa fimbo pado utashindwa kulifanya. Unaweza ukashawishiwa kufanya jambo ila kama haijakuingia na maamuzi ya kuona unaweza yakatoka kwako bado hutaweza kufanya.
Jambo lolote unalofikiria basi unaweza kulifikia kama ukiamua. Ukomo wa uwezo wako ni ul unaojiwekea mwenyewe kwenye fikra zako. Mawazo chanya yanaleta majibu chanya, na mawazo hasi yanaleta majibu hasi.
Maisha unayoishi sasa ni matokeo ya fikra zako, mambo yote unaypitia ni matokeo ya fikra zako. Kama unataka kuyabadili maisha yako anza kwanza kubadili fikra zako. Bila ya kubadili fikra utatumia kila njia ila bado hakuna kitakachbadilika, na kila mbinu utakayopewa utaona ni ngumu kwako ama labda wewe una bahati mbaya.
BADILI FIKRA, BADILI MAISHA