Kabla hujalala weka mipango ya siku ya kesho, jua ukiamka utafanya nini na nini. yaani siku nzima ya kesho ipange kabla hujalala hivyo utapoamka unajua ratiba yako ikoje. kufanya hivi kutakusaidia yafuatayo

1. itakupunguzia kupoteza muda

2. utakamilisha mipango ama malengo uliyoweka kwa siku hiyo

3. utafurahia kuamka kwa kuwa unajua kuna kitu cha muhimu unakwenda kufanya.

  Kuna sababu ya kisaikolojia inayohusisha upangaji wa siku inayofuata kabla ya kulala, kwa sababu akili yako itapitia mpango wako mzima na utapoamka itakuwa rahisi kwa wewe kuufuata. Fanya hivi na utaona tofauti kubwa kwenye utekelezaji wa mipango yako.