Binadamu wote tuna asili ya uvivu, hakuna mtu anaependa kuchoka, na kila mtu anapenda starehe ama mapumziko mazuri. Ugunduzi wote unaotokea duniani mpaka sasa ni njia za kutafuta jinsi ya kurahisisha kazi. Kazi ambazo zamani zIlikuwa zinafanyika kwa nguvu na watu wengi sasa zinafanyika na watu wa chache na wanatumia nguvu kidogo sana. Vitu siku hizi vimerahisishwa mpaka unaweza kushangaa huko tunakokwenda ukaweza ‘kudownload’ chakula kutoka kwenye mtandao, usibishe inaweza kutokea. Tuachane na hayo tuje kwenye hoja ya msingi, sote ni wavivu ila tuna mahitaji yetu, je nani atatutimizia? Hata tukirahisisha kazi kwa mashine gani bado anahitajika mtu aweze kuiendesha hiyo mashine. Kompyuta ina uwezo sawa na akili ya binadamu, inahifadhi taarifa, inahusisha kumbukumbu lakini bado haiwezi kufanya kazi bila ya kuendeshwa na binadamu.
Sasa unawezaje kuushinda uvivu ambao upo kwa asili? unawezaje kufurahia kuamka asubuhi na kwenda kufanya kazi? Ni rahisi sana kuushinda uvivu wako na njia ya kuushinda uvivu ni kuwa na malengo na mipango ambayo itakupatia mafanikio unayhitaji maishani. Ili uweze kuifurahia kazi ni lazima uweze kupata picha ya mafanikio utakayoyapata kutokana na kufanya kazi hiyo, sote tunafanya hivyo ila kwa nini bado wengine wanakuwa wavivu? Wengi wetu bado tunakuwa wavivu kufanya kazi kwa sababu hatujaweka malengo ama malengo tuliyoweka ni madogo hivyo hakuna ule msukumo wa ndani wa kuyafikia.
Ukiwa na malengo makubwa na ukiweza kuiona picha kubwa ya jinsi maisha yako na ya wanaokuzunguka yatakavyokuwa mazuri kwa wewe kufikia malengo yako, utapata msukumo kutoka ndani ya nafsi yako utakaokufanya uyafikie malengo yako. Kwa msukumo huo hata kazi unayoifanya hutaiona kama kazi bali njia ya kukufikisha kule unakotaka kwenda. Ukishaweza kuiona kazi kama sehemu ya maisha basi uvivu utakuwa mwisho kwako.
TAFADHALI WEKA MAONI YAKO HAPO CHINI KWA LOLOTE UNALOFIKIRI KUHUSIANA NA MADA HII. USIONDOKE BILA KUSEMA CHOCHOTE, MAONI YAKO NI YA MUHIMU SANA KWETU.
KAMA UMEIPENDA HII MADA TAFADHALI BONYEZA KIALAMA CHA FACEBOOK NA TWITTER KUSHOTO KWAKO KUWASHIRIKISHA RAFIKI ZAKO WA FACEBOOK NA TWITTER ILI UJUMBE HUU UWEZE KUWAFIKIA NA KUWABADILI WENGI. ASANTE SANA KWA USHIRIKIANO WAKO