Katika jamii unayoishi kuna changamoto nyingi sana kwa maisha kiujumla. Wanasema kuishi na watu kazi, ila hata wewe mwenyewe ni mtu hivyo wewe mwenye kuishi na mwenyewe ni kazi, si ndio?

watasema tuPICHA NA MUNCHED

  Katika jamii kuna watu wanaodhani wanajua sana na hivyo kujaribu kukosoa unalofanya na kudhani wanavyofanya ama wanavyofikiria wao ndio sahihi. Na hata ukiacha kufanya unalofanya na kufanya wanalokushauri wao kuna wengine watakaojitokeza na kukuambia unakosea ama umekosa mwelekeo. Kama huna malengo na mipango dhabiti ambayo umejipanga kwa ajili ya kuifikia ni rahisi sana kuyumbishwa na jamii. Hakuna utakalofanya kila mtu akuunge mkono. Ukiona kuna jambo unafanya na kila mtu anakuunga mkono asilimia 100(yani hakuna hata mmoja ana wasiwasi na wewe) basi acha kufanya hilo jambo mara moja kwa sababu linaweza kuwa hatari kwako.

  Kama unataka kufikia malengo uliyojiwekea basi kuna wakati inabidi uzibe masikio na usisikilize kelele za wanaokuambia huwezi ama haiwezekani. Kama unalolifanya ni jambo jema linalendana na sheria, mila na desturi basi wewe kaza mwendo kuelekea kwenye mafanikio. Ukitaka kila mtu akubaliane na wewe hakika hutofanya lolote kwenye maisha. Jamii imejaa watu wengi wanaokatisha tamaa, mashahidi wazuri watakaokushuhudia kwa nini huwezi ama utashindwa.

  Yapange maisha yako na elekea kwenye mipango yako, usisubiri kwenda na mkumbo wa jamii. Angalia wakosoaji wengi kwenye jamii wamefanikiwa kwenye nini? Hakuna jambo hata moja walilofanikiwa. Je unataka kuwa kama wao? Kama hutaki kuwa kama wao basi usiwasikilize.