MJASIRIAMALI MWENYE AFYA NI MJASIRIAMALI MWENYE FURAHA

  Kwenye maisha ya sasa yenye mihangaiko mingi kwa wengi wetu afya imekuwa kipaombele cha mwisho. Mihangaiko imekuwa mingi kiasi kwamba afya imekuwa sio kitu cha kufikiriwa sana. Inakuwa hivyo kwa sababu mabadiliko ya kiafya hayatokei mara moja ila kidogo kodogo afya inazorota na inafika sehemu ndio matatizo yanakuwa dhahiri ndipo watu tunaanza kuhangaika. Ili kuweza kufikia malengo yako uliyojiwekewa afya inabidi iwe kitu cha kwanza kukitunza kwa sababu bila afya njema ni vigumu kufanya kazi.

  Pamoja na majukumu mengi ya kikazi ama kijasiriamali tuliyonayo ni vyema tukajali afya zetu. Hizi hapa ni baadhi ya njia rahisi za kutunza afya yako bila ya kuathiri majukumu yako ya kila siku.

1. Kula vizuri. Ni muhimu kula mlo kamili ili kuwa na afya nzuri, kula protein ya kutosha, wanga ama sukari kidogo, mafuta kidogo(epuka mafuta ya wanyama, tumia ya mimea), mboga za majani na matunda. Kama wewe ni mlaji wa chipsi mayai kila siku basi afya yako iko hatarini.

mlo kamili

2. Kunywa maji mengi. Maji ni muhimu sana kwenye mwili wako, ili kuwa na afya njema ni vyema ukanywa maji mengi. Kujua faida za maji mwilini ambazo hazizungumziwi sana bongeza hapa

3. Pata usingizi wa kutosha. Pamoja na majukumu mengi uliyonayo hakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala. Inashauriwa kulala masaa 7-8 kwa usiku. Baadhi ya faida za usingizi wa kutosha ni;

  Inasaidia kungeza uwezo wako wa kutunza kumbukumbu

  Usingizi wa kutosha unaweza kukukinga na baadhi ya saratani.

  Pia kupata usingizi wa kutosha kunasaidia kupunguza uzito ama unene wa mwili.

4. Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara. Ni muhimu sana kufanya mazoezi, tena kama kazi yako ni ya kukaa kwa muda mrefu na kwenda na kurudi nyumbani unatumia usafiri, kama hufanyi mazoezi una hatari kubwa. Mazoezi sio lazima ukabebe vyuma(kama unaweza sawa) Unaweza ukaamua badhi ya siku ukatembea badala ya kupanda gari, kukimbia ama kuruka kamba. Kama kazi zako ni za kukaa unaweza kuweka utaratibu wa kuamka na kutembeatembea kidogo kila baada ya saa moja.

mazoezi kazini

Mazoezi yana faida nyingi, baadhi ya faida hizo ni;

  Kufanya mazoezi kunaweza kukukinga na baadhi ya saratani.

  Kufanya mazoezi kutakukinga na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

  Kufanya mazoezi kutakuongezea uwezo wa kulala na kupumzika vizuri.

  Hata kama huna muda kiasi gani jitahidi sana usikose muda wa kuitunza afya yako. Afya yako ni ya muhimu sana kushinda vitu vyote. Ijali sana.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: