Tunashauriwa kunywa maji ya kutosha ili kuwa na afya njema. Sehemu kubwa ya mwili wako ni maji. Kila seli kwenye mwili wako unahitaji maji ili kuchukua chakula na kutoa uchafu. Pia maji yanahitajika kwa usafirishaji mwilini, sehemu kubwa ya damu ni maji. Faida hizo zimezungumzwa sana na hivyo umesisitizwa kunywa maji walau lita moja na nusu kwa siku ili kuwa na afya njema. Kuna faida nyingine za maji ambazo huwa hazizungumziwi sana, na hizi hapa ni baadhi tu ya faida hizo

1. Kunywa maji kwa wingi kunakufanya uonekane kijana. Mwili wako ukiwa na maji ya kutosha inazuia ngozi kukunjamana na hivyo mtu kuonekana na ngozi nyororo hata kama umri umekwenda.

kunywa maji

2. Kupunguza uzito/unene. Kama hupendezwi na uzito ama unene wa mwili wako ukinywa maji mengi utapunguza uzito wako. Unywaji wa maji mengi unapunguza uzito wa mwili kwa sababu;

Ukinywa maji mengi unapunguza hamu ya kula hivyo hutoweza kula chakula kingi kinachosababisha uzito kuwa mkubwa. Pia maji yanasaidia uunguzwaji wa mafuta mwilini na kusidia kuondoa sumu mwilini.

3. Kujenga misuli. Mwili unapokuwa na maji ya kutosha unaweza kusambaza hewa ya oksijeni vizuri zaidi na hivyo misuli ya mwili inaweza kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchoka. Hii inasaidia kujenga misuli ya mwili.

4. Kuongeza akili, ndio unywaji wa maji unaongeza uwezo wa kufikiri na kuweka kumbukumbu. Hii ni kwa sababu maji yanasambaza chumvi zinazohitajika na seli za fahamu kwa ajili ya kusafirisha taarifa mbalimbali. Tafiti zinaonyesha kwamba ukinywa glasi 10 za maji unaongeza uwezo wa kufikiri kwa asilimia 30. Jaribu kama huamini.

5. Unywaji wa maji mengi unasaidia viungo kufanya kazi vizuri. Kunakuwa na majimaji ya kutosha kwenye viungo yanayozuia maumivu ya viungo.

  Kwa kifupi hizo ni baadhi tu ya faida za kunywa maji ya kutosha. Kiwang cha kunywa inabidi kisiwe chini ya glasi nane kwa siku. Kunywa maji utunze afya yako.