Wote tunaujua usemi unaosema tajiri ataendelea kuwa tajiri na masikini ataendelea kuwa masikini. Usemi huo una ukweli mkubwa sana ndani yake, na inachosababisha hali iwe hivyo ni kitu kimoja ambacho wengi hatukijui. Umewahi kusikia usemi kwamba tunakuwa kile tunachofikiri kwa muda mrefu. Yaani maisha yako ni matokeo ya fikra zako. Hii ndio sababu kubwa, FIKRA.

rich poor

  Tajiri anafikiria nini muda mwingi? Jinsi alivyopata utajiri, jinsi ya kuulinda na jinsi ya kuuongeza zaidi. Na ndicho kitakachotokea.

  Masikini anafikiria nini muda mwingi? Matatizo anaykumbana nayo, mambo yaliyomfanya awe masikini na kutafuta cha kulaumu. Matokeo yake anaendelea kuwa masikini.

PESA TZ

  Fikra zako zina nguvu kubwa sana kwenye maisha yako. Kile unachfikiri kwa muda mrefu ndicho kinachotokea kwenye maisha yako. Hivyo kama unatumia muda wako kuwaza juu ya matatizo yako utaendelea kupata matatizo zaidi. Badili fikra zako ili kubadili maisha yako.