Kwenye mtandao wa facebook kuna matapeli huwa wanawatumia watu ujumbe wa kutaka urafiki nao. Mara nyingi matapeli hao huweka picha ya mwanamke mrembo na hutuma ujumbe kwamba wamevutiwa na wewe na wanataka muwe wapenzi. Nadhani umewahi kupata ujumbe kama huo, mimi kila siku napata jumbe hizo na nimeshazizoea na huwa sihangaiki kuzifuatilia.

  Matapeli wa aina hii inasemekana wengi wanatokea Nigeria na jumbe zao nyingi wanazituma kwa lugha ya kiingereza.

scamscam2

  Juzi nimepata tena ujumbe huo ila huu ulinistua kidogo, tofauti na niivyozoea kupata ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya kiingereza, huo niliopata uitafsiriwa kwa kiswahii pia.

Conversation started Saturday
11:49pm
Marbel Johnson
hujambo wapenzi i am miss ya Marbel Johnson i ni nzuri sana kuangalia vijana, kutafuta kwa ajili ya upendo wa kweli Serious na nzuri sana na ya kueleweka mtu vijana kwamba anajua maana ya kweli ya upendo. Nilikwenda kwa maelezo yako na i kusoma na kuchukua riba ndani yake, tafadhali kama huna akili i mapenzi kama wewe kuandika mimi kwenye ID hii tafadhali hii ni anwani yangu ya barua pepe (marbeljohnson_o@ymail.com) Naamini umbali na umri haijalishi katika uhusiano mbaya lakini upendo mambo zaidi. matumaini ya kusikia kutoka kwenu hivi karibuni, na i na muhimu sana ya kujadili suala hilo na wewe. yako Marbel
°°°°°°°°°°°°°°°°°°° hello dear i am miss marbel johnson i am very good looking young, seeking for Serious true love with a very good and understandable young someone that knows the true meaning of love. I went through your profile and i read it and took interest in it, please if you don’t mind i will like you to write me on this ID please this is my email address ( marbeljohnson_o@ymail.com) I believe distance and age doesn’t matter in a serious relationship but love matters most . hoping to hear from you soon,and i have very important issue to discuss with you . yours marbel

  Hii iinifanya nifikiri kwa muda, kwa nini wameamua kutafsiri? Nikapata wazo kwamba baada ya kuona sijibu wameona wabadili mbinu za kunifikia huenda walihisi sielewi kiingereza hivyo wakabadili na kutumia kiswahili.

  Kama mpaka matapeli ni wabunifu inakuwaje wewe unashindwa kuwa mbunifu? Ubunifu ndio njia pekee ya kukutofautisha wewe na wengine na ndio njia nzuri itakayokufanya uweze kufikia ndoto na malengo yako bila matatizo.

  Kwa lolote unalofanya hakikisha unatumia ubunifu wa kipekee ili uweze kupata matokeo bora. Kila mtu ni mbunifu ni wewe tu kuamua kuanza kutumia ubunifu wako.