Kwako msomaji na mfuatiliaji wa makala mbalimbali kwenye blog ya AMKA MTANZANIA. Blog yetu imeshika nafasi ya pili kwenye kipengele cha BEST BUSINESS BLOG kwenye shindano la blogs tanzania.

blog award

  Ushindi huu umetokana na wewe msomaji kupiga kura na kuwashirikisha wengine nao wakapiga kura.

  Napenda kutoa shukrani za dhati kwa wasomaji wote wa blog hii. Kushika nafasi hiyo kunatoa moyo kwamba kuna watu wanafuatilia na wanafaidika na blog hii.

  Naomba tuendelee kuwa wafuatiliaji wa blog hii na pia tuwaalike marafiki zetu wa kwenye mitandao nao wafuatilie blog hii.

  Nawapenda sana wasomaji wote, naipenda sana Tanzania na nina imani siku moja Tanzania itasimama baada ya kila mtanzania kuamka na kujua nafasi yake na uwezo wake.

  Tuendelee kushirikiana kwa mambo mbalimbali yatakayotuwezesha kufikia malengo yetu na kufanikiwa kwenye maisha.

  ASANTE SANA NA KARIBU NA UWASHIRIKISHE WENGINE.

Matokeo ya Tanzanian Blog Awards (2013)