Kama nilivyoahidi kutuma kitabu cha njia 100 za kujihamasisha, natekeleza ahadi hiyo. Katika makala ya HIKI NDICHO UNACHOTAKIWA KUFANYA KILA SIKU ILI UFANIKIWE(kama hujaisoma bonyeza hayo maandishi kuisoma) tuliona umuhimu wa kujihamasisha kila siku ila kuweza kuwa na siku yenye mafanikio na furaha.
Tuliona njia mbali mbali za kujihamasisha kila siku na baadhi ya njia hizo ni kujisomea vitabu vya kuhamasisha na kusikiliza vitabu vilivyosomwa(AUDIO BOOKS)
Kwa utaratibu wa kujisomea vitabu nimekuwa nikituma vitabu bure kwa wanachama wote wa mtandao huu na mpaka sasa nimeshatuma vitabu zaidi ya 10 kwa watu zaidi ya 500. Na hapa nitatuma kitabu kinachoelezea njia 100 za kujihamasisha na kubadili maisha yako.
Kwa upande wa vitabu vilivyosomwa (AUDIO BOOKS) ninatoa memory card(2GB) yenye vitabu 25 vizuri sana na vinavyohamasisha na kubadili maisha. Memory card hiyo inapatikana kwa TSH 15,000/= tu. Kujua vitabu vilivyopo kwenye kadi hiyo na maelezo mengine tafadhali bonyeza HAPA.
Kutokana na uvivu wa wengi unaopelekea kushindwa kusoma vitabu mpaka mwisho hivyo kukosa vitu vizuri, nimejitahidi kutafuta kitabu hiki katika mifumo miwili. Kuna kitabu kamili ambacho kina kurasa 151, na kuna muhtasari(summary) wa kitabu hicho wenye kurasa 17.
Kama ukiweza kukimaliza kusoma kitabu utapata mengi sana, na kama utashindwa kabisa basi angalau usome huo muhtasari bado utapata vitu vingi vitakavyobadili maisha yako. Hata kama upo bize kiasi gani huwezi kukosa muda wa kusoma kurasa 17 tu. Tafadhali sana fanya hivyo kwa ajili ya maisha yako mwenyewe.
Kwa kuwa njia hizo ziko 100 na kila moja imeelezewa kwa kujitegemea sio lazima kumaliza kukisoma kitabu ndani ya siku moja(au chache). Unaweza kuweka lengo la kusoma njia kumi(au ukishindwa 5) kila siku asubuhi au jioni na ndani ya wiki mbili utakuwa umemaliza njia zote 100.
Naweka link mbili za vitabu hivyo(kitabu kamili na muhtasari). Bonyeza maandishi hayo hapo chini kudownload vitabu hivyo. Kupata vyote viwili bonyeza link moja na baadae ubonyeze nyingine.
100-ways-to-motivate-yourself(kitabu kamili kurasa 151)
100-ways-to-motivate-yourself(muhtasari kurasa 17)
Karibu sana tuendelee kuhamasishana na kujihamasisha wenyewe. Pia waalime marafiki zako watembelee blog(AMKA MTANZANIA) na kujiunga na mtandao huu ili nao wapate mambo yaha mazuri.
Kumbuka UMELETWA DUNIANI KUFANYA MABADILIKO, fanya jambo lolote hata liwe dogo kiasi gani bali ubadili hali iliyopo na kuwa bora zaidi.
Nakutakia kila la heri katika safari yako ya mafanikio na mabadiliko.
KAMA BADO HUJAJIUNGA NA MTANDAO HUU JIUNGE KWA KUBONYEZA HAPA NA KUANDIKA EMAIL YAKO. KWA KUJIUNGA UTAPATA VITABU MBALIMBALI VYA KUJIENDELEZA NA KUJIHAMASISHA.