Katika makala ya kujihamasisha kila siku, tuliona umuhimu mkubwa wa kujihamasisha kila siku ili kuweza kuwa na siku yenye mafanikio na hatimaye kufikia malengo tuliyojiwekea.(kama hujaisoma bonyeza maandishi haya kuisoma)

  Tuliona njia mbalimbali za kujihamasisha kila siku na baadhi ya njia hizo ni

1. Kujisomea vitabu vinavyohamasisha na kuelimisha. Kwa njia hii niwekuwa nikituma vitabu mara kwa mara kwa wanachama wa mtandao huu.

2. Kusikiliza vitabu vilivyosomwa (AUDIO BOOKS).

3. Kutembelea mitandao mbalimbali inayotoa mazungumzo ya kufundisha na kuhamasisha.

50

  Hapa nataka tuzungumzie zaidi jinsi ya kutumia mitandao hii na urahisi wa wewe kufanya hivyo.

  Kuna mitandao mingi inayoweka video zenye mafundisho ya kuhamasisha na kuelimisha. Ila kwa kuanzia tutaangalia mitandao miwili.

1. YOUTUBE

  Youtube ndio mtandao mkubwa wa video duniani. Kuna video nyingi sana Youtube hivyo kutokujua unachotafuta unaweza kujikuta unaishia kuangalia video za muziki.

  Hivyo unapotembelea youtube unaweza kusearch mada unayotaka kujifunza kisha ukapata video za kutosha.

  Kwa kujihamasisha anza kwa kutafuta majina haya na utapata video nyingi nzuri za kuanzia, ZIG ZIGLER, ANTHONY ROBBINS, JACK CONFIELD, ROBIN SHARMA, EARL NIGHTINGALE, BOB PROCTOR, BRIAN TRACY, ROBERT KIYOSAKI.

  Kwa kuanzia na majina hayo utapata video zenye mafundisho mazuri na yanayohamasisha. Na kupitia hapo utapata mafundisho mengi zaidi.

2. TED TALKS

  Huu ni mtandao maalumu kwa lengo la kuhamasisha watu katika maswala ya ubunifu, teknolojia na burudani. Kwenye mtandao huu kuna video zaidi ya 1,000 zenye mafundisho mazuri na yanayohamasisha. Video za kwenye mtandao huu zimepangwa kutokana na topic mbalimbali hivyo ukishachagua topic utakutana na video zinazohusika na topic hiyo. Kwa kuanzia unaweza kuangalia video zilizoangaliwa na watu wengi zaidi na baadae ukafatilia zile zinazokupendeza zaidi. Kwa kuanzia unaweza kufuatilia video hizi 100 ambazo mdau mmoja aliziangalia na zikamsaidia sana. Bonyeza hapa kupata maelezo ya video hizo 100.

  UNAWEZAJE KUANGALIA MAZUNGUMZO HAYA KWA MTANDAO BILA YA KUINGIA GHARAMA KUBWA?

  Kama tunavyojua gharama za mitandao ni kubwa sana hasa linapokuja swala la kuangalia video online au kudownload. Na ili ufaidi video za mazungumzo haya ni vyema ukazidownload ili kuweza kuziangalia bila kukata kata.

  Kupunguza gharama za mtandao na kupata mtandao wa uhakika usio na kikomo, kuna mpango mzuri wa kupata mtandao wa uhakika usio na kikomo.

  Kwa malipo kidogo tu ya tsh 15,000/= unaweza kupata mtandao usio na kikomo kwa mwezi mmoja. Kupata maelezo zaidi kuhusu mtandao huo tafadhali bonyeza HAPA.

  Jitahidi sana kabla ya kuianza siku yako kupata TED TALK moja na siku yako itakuwa nzuri sana. Uzuri wa mazungumzo haya hayachukui zaidi ya dakika 20.

  Jinsi unavyoishi siku yako moja kwa mafanikio ndivyo unavyotengeneza mafanikio maishani.