Mwaka 2014 bado ni mchanga na watu wengi bado wana matarajio makubwa sana kwa mwaka huu. Ukitembelea mitandao mbalimbali hasa ya kijamii unaona watu wakiweka mipango mbalimbali ya mwaka huu 2014. Wengi wanatarajia mambo na mabadiliko makubwa sana mwaka huu. Ni kitu kizuri sana kuwa na matazamio makubwa kwenye maisha, ila kuna tatizo moja ambalo hujitokeza kila mwaka.![]()
Mpaka huu mwezi wa kwanza utakapokwisha asilimia 80 ya watu watakuwa wameshasahau malengo waliyojiwekea, asilimia 90 watakuwa wamesharejea tabia walizopanga kuacha na asilimia kubwa watakuwa hawana tena huu ‘mzuka’ wa mabadiliko walioko nao sasa. Fikiria miaka iliyopita na waangalie wanaokuzunguka utaona dhahiri ni jinsi gani mambo haya yanatokea.
Huenda nawe ni mmoja wa wahanga wa hali hii. Hali hii inatokea kwa watu wengi sana kwenye jamii zetu na kwa kuwa watu hukubaliana nayo ndio chanzo kikuu cha kuwa na maisha yale yale kila mwaka ambayo hawayafurahii. Kama na wewe umechoshwa na maisha hayo ya kila mwanzo wa mwaka kupanga na baadae mipango inayeyuka, usihofu tena maana jibu umeshalipata.
AMKA MTANZANIA imeandaa semina ya kubadili maisha yako mwaka 2014 itakayofanyika jumamosi tarehe 18/01/2014.
Mada zitakazozungumzwa ni;
1. Wewe ni zaidi ya unavyojijua.
2. Wewe ndiye kiongozi mkuu wa maisha yako.
3. Umuhimu wa kujihamasisha na kujiendeleza binafsi.
4. Jinsi ya kuweka malengo makubwa na utakayoyafikia.
5. Makosa makubwa unayofanya wakati wa kuweka na kutimiza malengo yako na jinsi ya kuyaepuka.
Semina itafanyika UBUNGO PLAZA, kwenye ukumbi wa chuo cha INFOBRIDGE(MUGEREZI SPACIAL TECHNOLOGY)
Kiingilio ni TSH 10,000/= Muda ni kuanzia saa nne kamili asubuhi mpaka saa nane kamili mchana.
Bonyeza link hii http://bit.ly/1aawKcL kujaza fomu ya kuhudhuria.
Usikose kuhudhuria semina hii itakayobadili maisha yako na kuwa na maisha utakayoyafurahia kila siku.
Njoo wewe na wale unaowapenda na kuwajali kwenye maisha ili muweze kuwa na maisha bora.
Ufanye Mwaka 2014 Kuwa Mwaka wa Mabadiliko Makubwa Kwenye Maisha Yako.