Ili kuweza kufungua blog yako kwa kutumia blogger ni lazima uwe na google akaunti.
1. Kama tayari una google account(kama unatumia gmail) unaweza kutumia akaunti hiyo kufungulia blog.
2. Kama hutaki kutumia akaunti hiyo ama huna akaunti ya google unaweza kusajili akaunti mpya kwa hatua zifuatazo.
a. Nenda www.accounts.google.com itakuja kurasa kama inayoonekana kwenye picha hapo chini
sign in
kama tayari unatumia gmail na unataka kutumia akaunti hiyo hiyo kuendesha blog basi bonyeza sehemu ya sign in na uingie.
kama huna akaunti ya google ama unataka kutengeneza akaunti nyingine jaza hizo taarifa zinazohitajika.
kuingia1

kuingia2
b. Baada ya kuingiza taarifa bonyeza agree google terms kisha bonyeza next step
c. Kama hukuweka email nyingine unayomiliki utatakiwa kuthibitisha akaunti yako kwa njia ya simu.
tengeneza
weka namba yako ya simu ukianza na +255(au chagua tanzania kisha anza namba na 0) kisha watakutumia code ambayo utaiingiza hapo hapo na kuendelea.

c. Ukishaingiza code na kubonyeza continue, watakuletea ujumbe kwamba akaunti yako iko tayari.
 tayari
Baada ya hapo unaweza kwenda kwenye GMAIL na ukakuta email za ukaribisho.

KAMA HUJAWAHI KUWA NA AKAUNTI YA GOOGLE JUA FAIDA NYINGI ZA KUWA NA AKAUNTI YA GOOGLE.
Kwa akaunti moja ya google unaweza kutumia vitu vifuatavyo;
1. Unatumia GMAIL kutuma na kupokea email
2. Unaweza kutumia BLOGGER kuendeshea blog zako(unaweza kuwa nazo nyingi kwa akaunti moja)
3. Unaweza kutumia YOUTUBE kuweka video zako
4. Unaweza kutumia GOOGLE DRIVE kuhifadhi document zako online
5. Unaweza kutumia ADSENSE kuweka matangazo kwenye website au blog zako
6. Unaweza kutumia GOOGLE+ kama mtandao wa kijamii.
Na faida nyingine nyingi.
gmail

Mpaka kufikia hapo utakuwa umeshafungua akaunti yako ya google. Kama utakwama popote usisite kuweka maoni yako hapo chini.