Kama hutokuwa na vitu vya kukurahisishia kazi unaweza kuwa unachoka sana na kushindwa kufikia malengo yako.
Hapa nitaeleza program tatu muhimu ambazo wewe kama blogger unahitaji kuwa nazo ili kurahisisha kazi yako.
1. Windows Live Writter.
Hii ni program ya kuandikia na kuedit post ukiwa offline. Kama unavyojua kwenye blogger na hata wordpress ili uweze kuandika na kupost inakubidi uwe kwenye mtandao. Kwa kutumia program hii unaweza kuandika post na kuedit kwa kuweka picha, links na hata video bila ya kuwa online. Unaweza kusave kazi zako offline na unapokuwa online ukazipost tu. Hivyo kama unapata muda wa kuwa online dakika tano unaweza kupost post tano.
Hata post hii naiandika kwenye windows live offline kama inavyoonekana hapo chini.![]()
Faisa nyingine kubwa ya program hii ni kwamba unaweza kuitumia kuendesha blog zaidi ya moja. Kama unaendesha blogs nyingi unaweza zote kuziweka hapo na ukachagua ni ipi unataka kuiandika kwa wakati huo. Kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini nimeweka blog tatu kwenye windows live, KISIMA CHA MAARIFA, MAKIRITA AMANI NA AMKA MTANZANIA ![]()
Program hii inapatikana bure na unaweza kuidownload kwa kubonyeza hapa
2. Evernote
Kama wewe unaendesha blog ya kuandika, yaani habari zako unaandika mwenyewe na sio kukopi ama kuchukua kwa wengine basi ni muhimu sana ukawa na program ya kutunza mawazo yako. Mara nyingi unaweza kuwa mahali na ukawa mbali na komputa yako ila likakujia wazo la kuandika. usipolihifadhi wazo hilo vizuri unajikuta limeshapotea(nadhani hii imeshakutokea mara nyingi sana).
Program ya evernote inakuwezesha kuhifadhi mawazo yako ya kuandika online hivyo unaweza kuyafikia wakati wowote na popote ulipo. Kama unatumia smart phone unaweza kuwa na application ya program hii kwenye simu yako na pia kuwa na program hii kwenye computer yako. Unaweza kuyafanyia kazi mawazo yako ukiwa kwenye computer au kwenye simu cha msingi ni uwe na mtandao.![]()
![]()
Program hii inapatikana bure na pia kuna ya kulipia. kudownload program hii bonyeza hapa
Kupata aplication ya smart phone kama unatumia android nenda google play kisha search evernote upande wa apps.
3. Blogger/Wordpress apps
Kama una smart phone basi unaweza kurahisisha kazi yako ya blogging kwa kutumia simu yako ya mkononi. Kuna baadhi ya blogs zangu huwa na update nikiwa kwenye foleni au nasubiri kitu fulani.
Ili uweze kutumia smart phone yako kuendesha blog yako nenda google play na usearch blogger(kama unatumia blogger) au wordpress(kama unatumia wordpress) na kisha install application hiyo kwenye simu yako.
Ukishaweka app hiyo inaweza kuwa rahisi kwako kuandika, kuedit na kupost popote ulipo na simu yako.
Natumaini kuna kipya umejifunza hapa na utaanza kutumia mara moja kurahisisha kazi zako za blogging.
Kama utakwama popote kwenye kupata au kutumia program hizo tafadhali weka maoni yako hapo chini.