Hili Ndio Kosa Kubwa Unalofanya Kila Siku Linaloathiri Uzalishaji Wako.

  Katika shughuli yoyote unayofanya uzalishaji ndio jambo la msingi sana. Kuweza kukaa chini na kufanya kazi halafu ukatoa majibu mazuri ni jambo litakalokufanya uridhike na kuifurahia kazi unayofanya.

  Ili uweze kufanikiwa kwenye kazi au biashara unayofanya ni muhimu sana kutoa majibu mazuri yanayokupendeza wewe na wale wanaotumia majibu hayo. Uzalishaji wako ni kipimo cha msingi sana kama utafanikiwa kwenye shughuli unayofanya au hutofanikiwa.

  Pamoja na uzalishaji kuwa kitu cha muhimu kwenye kazi yoyote, ni watu wachache sana wenye uzalishaji wa hali ya juu kwenye kazi zao. Wengi wamechoshwa na kazi zao na hata wajitahidi vipi kufanya kazi bado uzalishaji wao unakuwa wa chini sana.

DSC02836

  Je wewe ni mmoja wa watu ambao wanapambana kuongeza uzalishaji wako ila unashindwa? Je unafanya kazi kwa muda mrefu ila hupati majibu unayotegemea? Kama jibu ni ndio, una tatizo la uzalishaji. Unaweza kuwa umeweka malengo na mipango yako vizuri na ukaweka ratiba ya siku ila mwisho wa siku huoni ulichozalisha. Unaona unafanya kazi nyingi sana na kubwa ila ukiangalia ulichozalisha hakiendani na kiwango cha kazi uliyofanya.

  Haya yote yanatokana na tatizo moja, hufanyi kazi wala hupumziki, upo upo tu. Hili ndio kosa kubwa unalofanya kila siku ambalo linaathiri uzalishaji wako. Unafikiri unapumzika kumbe hupumziki, unafikiri una fanya kazi kumbe hufanyi kazi. Unakosa vyote, yaani mapumziko na kazi hivyo unakuwa katika hali mbaya sana. Unachoka sana na unaona kazi unayofanya ni mzigo mkubwa sana kwako.

  Inakuwaje hufanyi kazi na wala hupumziki?

  Kinachotokea ni kwamba unafanya kazi, ila wakati unafanya kazi mawazo yako hayapo kwenye kazi unayofanya. Mawazo yako yanakuwa kwenye kupumzika au nyumbani au sehemu nyingine yoyote mbali na kazi unayoifanya. Unapofika wakati unapumzika mawazo yako yanakuwa hayapo kwenye mapumziko yako bali yapo kwenye kazi yako. Unafikiria ni jinsi gani unaweza kuboresha kazi yako au ni jinsi gani unashindwa kuwa na uzalishaji wa kutosha. Kwa kuweka mawazo yako mbali na unachofanya kunakufanya ushindwe kufurahia unachofanya iwe ni kazi au mapumziko.

  Wakati mwingine unafanya kazi kwa muda mrefu sana na unakosa mapumziko ya kutosha hivyo mwili unachoka sana. Mwili unapochoka sana uzalishaji wako pia unapungua.

 

  Ufanye nini kuepukana na hali hii ya kuwa na uzalishaji kidogo?

  Kuna mambo mengi unaweza kufanya na yakakusaidia kuongeza uzalishaji wako na ukaanza kuifurahia kazi yako. Baadhi ya mambo hayo ni;

1. Pangilia shughuli zako kabla hujaanza kufanya. Mara nyingi unapoteza muda mwingi kwenye kazi ndogo kutokana na kukosa mipango.

2. Panga muda wa kufanya kazi na muda wa kupumzika. Baada ya kujua ni nini unataka kufanya weka muda utakaofanya kazi na muda utakaopumzika.

3. Weka akili yako kwenye jukumu unalofanya. Unapofanya kazi weka akili yako yote kwenye kazi unayofanya. Unapopumzika weka akili yako yote kwenye mapumziko yako. Hii itakufanya ufurahie kile unachofanya na uweze kuwa na uzalishaji mkubwa.

  Katika jambo lolote unalofanya weka mawazo yako yote kwenye jambo hilo. Wacha kuhofia jana au kesho, hebu furahia wakati huo unaofanya jambo hilo na utaona ni jinsi gani itakuwa rahisi kufanya jambo hilo.

  Japokuwa ni muhimu kuweka akili yako yote kwenye jambo unalofanya kwenye wakati husika bado sio rahisi kufanya hivyo. Unapokaa na kuanza kufanya jambo lolote yataanza kukujia mawazo ya mambo yaliyopita au mawazo na hofu za siku zijazo. Pia unaweza kukuta mawazo umeyaweka kwenye mawasiliano, labda unasubiri kupigiwa simu. Kama kufikiria jambo moja unalolifanya na kuacha mengine ni vigumu kwako kuna njia moja unaweza kuitumia kuielekeza akili yako ikae sehemu moja. Njia hiyo ni meditation(soma; umuhimu wa kufanya meditation) Kwa kufanya meditation utaweza kuyatuliza mawazo yako sehemu moja na kupata majibu mazuri ya chochote unachofanya.

  Siri kubwa ya kuongeza uzalishaji ni; fanya kazi unapofanya kazi na pumzika unapopumzika.

 PICHA ILIYOTUMIKA KWENYE MAKALA NILITUMIWA NA MSOMAJI WA BLOG HII KUTOKA NAIROBI KENYA BWANA SALIM SALEH. ALIPIGA PICHA HII ALIPOTEMBELEA TANZANIA MWISHONI MWA MWAKA JANA. KAMA UNA PICHA ZINAZOWEZA KUTUMIKA KWENYE BLOG HII USISITE KUNITUMIA. ASANTE.

One thought on “Hili Ndio Kosa Kubwa Unalofanya Kila Siku Linaloathiri Uzalishaji Wako.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: