Kwenye makala ya blogger iliyopita tuliona jinsi unavyoweza kubadili template ya blog yako na kuifanya iwe na muonekano mzuri zaidi. Pia niliweka link mbalimbali ambapo unaweza kudownload template nzuri bure kabisa. Baadae tulikwenda hatua kwa hatua kuibadili template. Kama ulikosa mafunzo haya bonyeza maandishi haya.

Leo tutaangalia kufanya marekebisho kwenye template uliyoweka.

Kama umeangalia kwa makini baada ya kubadili template kuna vitu vingi vinaonekana kwenye template ambavyo hutaki viwepo. Kwa mfano kama kuna sliding picture unaweza kutaka kuzitoa au kubadili na uweke za kwako. Pia baadhi ya link zinazooonekana kwenye template yako mpya zinakuwa sio sawa na unazotaka wewe.

Jinsi ya kufanya marekebisho kwenye template.

1. Hatua ya kwanza kabisa unapouzzip au kuextract template uliyodownload utaona file limeandikwa READ ME

Fungua file hili na utaona maelekezo ya sehemu unazotakiwa kubadili.

template1

Kama huna file hili usiwe na shaka, endelea mbele.

2. Nenda kwenye blogger kisha chagua blog unayotaka kuifanyia marekebisho. Bonyeza sehemu ya template utaona kitu kifuatacho.

2

Bonyeza sehemu iliyoandikwa EDIT HTML kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu. Utaona picha kama hiyo hapo chini.

templates2

3. Bonyeza katikati ya hayo maandishi mengi na hakikisha cursor ipo ndani ya hayo maandishi popote pale. Baada ya cursor kuwa ndani ya maandishi bonyeza CTRL na F kwenye keybord yako. Yaani bonyeza control na key F. Itatokea sehemu ya search kama hiyo picha hapo chini.

templates3

4. Tumia sehemu hii ya search kubadili kitu chochote ambacho kinaonekana kwenye template yako. Kwa mfano kama unataka kubadili menu iliyoandikwa DOWNLOAD na uipe jina lingine weka hapo kwenye search neno download kisha itakupeleka moja kwa moja kwenye link ya menu hiyo.

5. Kama unataka kubadili sliding pictures(picha zinazobadilika kwenye template) au unataka kuziondoa kabisa nenda sehemu ya search kisha andika neno SLIDER au neno jingine linaloonekana juu ya kicha hizo katika template. Moja kwa moja itakupeleka zilipo codes za slide na watakuonesha idadi ya sliders kulingana na idadi ya picha zinazobadilika.

6. Kubadili picha badili url ya picha iliyopo kwenye template na kuweka url ya picha zako. URL ya picha inaonekana kama ifuatavyo; http://lh3.ggpht.com/-kzt6QH1xlNQ/Uz2vuECZ0SI/AAAAAAAACNU/TqLgwXiy86A/1._thumb%25255B1%25255D.jpg badili url hiyo kwa kuihighlight na kuweka url ya picha yako.

7. Kama hujui jinsi ya kupata url ya picha yako, chukua picha unayoitaka kisha i-upload kwenye post kwenye blog yako kisha fungua post yako na RIGHT CLICK kwenye picha unayotaka kupata url yake kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa COPY IMAGE LOCATION kama inavyoonekana hapo chini;

templates4

8. Unaweza kuendelea kubadili vitu vingi uwezavyo kadiri ya mapendeleo yako.

 

TAHADHARI;

1. Hizo unazoona ni CODES yaani sheria za programing. Ukifuta vitu hovyo utaharibu template yote.

2. Kulingana na maelezo ya funzo hili badili neno husika au link husika tu, usifute wala kuongeza hizi codes.

3. Ukikuta vitu vimefungwa kwenye mabano kama <> au </> viache hivyo hivyo.

4. Ukitaka kujua zaidi jinsi ya kubadili codes hizi unahitaji kujifunza basics za programing. Ni rahisi sana ila kutokana na wingi wake sitoweza kuzifunsisha kwenye blog hii.

5. Kuna kitabu cha kiswahili kimeandikwa kinachoelezea hizi codes na kinauzwa kwa soft copy. Kama utahitaji kitabu hicho wasiliana nami na nitakuunganisha na muuzaji wa kitabu hiko. Tumia mawasiliano yangu ambayo ni 0717396253/amakirita@gmail .com

Karibu sana kwa maoni, ushauri na mapendekezo.