Kama Unafanya Mambo Haya Matano Huna Maisha.

Kwa binadamu yeyote yule thamani ya maisha yake huwa inatokana na mafanikio aliyofikia au thamani anayoiongeza kwenye maisha yake na maisha ya watu wengine. Mafanikio sio lazima yawe ya kifedha bali hata kuweza kufanya kitu ambacho watu wengine watakithamini na kufurahi wewe kuweza kubadili maisha yao.

  Watu wengi sana wanasongwa na msongo wa mawazo kutokana na kushindwa kuboresha maisha yao na ya wale wanaowazunguka. Hali hii inawafanya kuona maisha yao hayana thamani na kuamua kufanya tu jambo lolote ambalo linatokea mbele yao. Ndio maana wengine wanaishia kuwa walevi na hata kutumia mihadarati na wengine wanaenda mbali zaidi mpaka kukatisha maisha yao.

  Kuna tabia nyingi sana ambazo watu wanapenda kuzifanya kwenye maisha yao ya kawaida na zinawafanya kupoteza thamani ya maisha yao. Hapa nitazungumzia mambo matano ambayo inawezekana na wewe unapenda kuyafanya ila hujajua kama yanakuzuia wewe kuboresha maisha yako.

1. Unapoteza muda mwingi kufanya mambo ambayo hayana msaada kwenye maisha yako.

  Jambo la kwanza kabisa ni muda, sio fedha, muda. Ukipoteza mamilioni ya fedha unaweza kutengeneza mengine, ukipoteza sekunde moja ya muda huwezi kuipata tena.

  Kuna mambo mengi sana ambayo unapenda kutumia muda wako kuyafanya lakini hayana msaada wowote kwenye maisha yako. Muda unaotumia kuangalia vipindi vingi vya tv, kuingia kila mtandao wa kijamii kujua watu wanafanya nini, kufuatilia habari za udaku, kufuatilia maisha ya watu ni muda ambao umeamua kuupoteza bure.

  Kama umeweka malengo na mipango kila wakati jiulize je hili ninalofanya litanisaidia kufikia malengo yangu? Kama jibu ni hapana acha kufanya jambo hilo mara moja.

kitabu kava tangazo

2. Unalalamika sana.

Kama kila kitu kinachotokea kwenye maisha yako wewe ni kulalamika tu basi huna maisha. Kwa sababu walalamikaji wengi sio wachukua hatua. Utalalamika sana baadae utaacha na maisha yako yataendelea kuwa kama yalivyokuwa. Kama kimetokea kitu ambacho hakikuridhishi usilalamike, chukua hatua, hiyo ndio njia pekee ya kuboresha maisha yako.

3. Hulishi akili yako.

Kama hakuna habari nzuri unazoingiza kwenye akili yako basi huna maisha na unapotea kabisa. Kama taarifa unazopata ni habari za udaku na kufuatilia maisha ya watu ni vigumu sana kuboresha maisha yako. Kuwa na utaratibu wa kujisomea vitabu na kutembelea mitandao inayofundisha kama huu AMKA MTANZANIA. Kama bado hujajiunga na amka mtanzania jiunge leo ili uwe unatumiwa vitabu vya kulisha akili yako.

4. Huna malengo na mipango ya maisha yako.

Kama unaendesha tu maisha bila ya kuwa na malengo nasikitika kukuambia kwamba hujui unakokwenda na huna maisha. Kwa kutokuwa na malengo utajikuta unatumia muda wako kufanya mambo ambayo hayana msaada kwako na pia utajikuta unalalamika kila wakati. Weka malengo kwenye maisha yako na kisha anza kuyatimiza malengo hayo. Kama hujajua jinsi ya kuweka malengo bonyeza hapa na usome makala zinazohusiana na malengo.

5. Unatumia fedha kwenye mambo ambayo siyo ya msingi.

Sio kila kitu unachotaka kununua ni hitaji la msingi. Kuna mahitaji ya msingi na mahitaji ya anasa. Vitu kama chakula malazi mavazi na afya ni vitu vya msingi sana ambavyo unatakiwa kuvigharamia. Ila inapokuja unataka vya ufahari zaidi hakikisha unatengeneza kipato cha kuweza kumudu huo ufahari. Kama bado kipato chako ni kidogo acha kutumia fedha kwenye vitu ambavyo sio vya msingi. Kutaka kununua matoleo mapya ya simu, kutaka kununua kila nguo mpya inayotoka au mambo mengine ya kuonekana ni matumizi mabovu sana ya fedha zako. Mwisho wa siku unanunua vitu ambavyo havina matumizi makubwa kwako na unabaki na msongo wa mawazo kutokana na tatizo la fedha.

  Kama unafanya mambo haya matano hakuna njia yoyote unayoweza kutumia ukafanikiwa kama hutoacha tabia hizo. Anza kubadili tabia zako ili uboreshe maisha yako.

  Kwa kujua tabia nyingine ishirini zaidi zinazokuzuia wewe kufikia mafanikio jipatie kitabu KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIO TAJIRI na ujifunze tabia hizi unazotakiwa kuziacha mara moja. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu hiki.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s