Dunia Inabadilika Kwa Kasi Sana, Fanya Hivi Ili Usipitwe Na Mabadiliko Haya.

Tunaishi kwenye zama ambazo mabadiliko mengi sana yanatokea na pia yanatokea kwa kasi kubwa sana. Vitu ambavyo vilikuwa vinaonekana ni vya kisasa miaka mitano iliyopita hivi sasa ni vitu vya kawaida kabisa na haviwashangazi tena watu. Miaka mitano iliyopita kusikiliza muziki kupitia CD ilionekana ni teknolojia kubwa ila kwa sasa hakuna hata anayeishangaa sana CD, kuna memory kadi ndogo zaidi na zinazobeba miziki mingi zaidi.

  Mabadiliko haya pia yametokea kwa kasi kubwa sana kwenye mtandao wa internet na yamekuwa na athari kubwa sana kwenye biashara. Miaka kumi iliyopita kufanya kazi kwenye ofisi ilikuwa ufahari mkubwa sana ila sasa hivi kila mtu anakimbilia kufanyia kazi nyumbani na ikiwezekana kitandani. Ni kitu gani kimewezesha mabadiliko yote haya?

pesa mtandao

  Ukuaji wa mtandao wa intaneti umeleta mabadiliko makubwa sana kwenye kazi na biashara. Biashara zote zilizoweza kutumia mtandao wa intanet vizuri zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. Watu wengi wameweza kufanyia kazi zao nyumbani na kuingiza kipato kikubwa kupitia mtandao wa intaneti.

  Je wewe umeshajua mbinu za kutengeneza fedha kwa kutumia mtandao? Kwa kazi au biashara yoyote ambayo unafanya, unaweza kutengeneza kipato kisicho na kikomo kupitia intaneti.

  Kwa mfano kama unafuga kuku, unaweza kuwa na blog yako ambayo unaandika mbinu mbalimbali unazotumia katika ufugaji wako. Kupitia mtandao kuna mtu naye atakuwa anatafuta mbinu za ufugaji wa kuku na kwa kutafuta atafikia kwenye blog yako. Baada ya muda unakuta wafugaji wengi wanafuatilia blog yako ili kupata taarifa mbalimbali za ufugaji. Baada ya kuwa na watu wengi hawa unaweza kuwauzia kuku, mayai na hata bidhaa nyingine kupitia blog yako. Pia unaweza kutoa mafunzo yaliyoingia ndani zaidi na kutoza ada kidogo, au unaweza kuandika kitabu kinachoelezea ufugaji kwa undani na ukawauzia wasomaji wako kwa gharama ndogo. Kwa njia hii kama una wasomaji wengi unaweza kutengeneza kipato kisicho na kikomo kwa sababu kila siku wasomaji wataongezeka na watataka elimu na bidhaa zaidi kutoka kwako.

  Mfano huo unaweza kuutumia kwenye biashara yoyote au kazi yoyote unayofanya. Hata kama umeajiriwa unaweza kutumia blog kuandika mambo yanayohusiana na ujuzi wako au vipaji vyako. Kwa njia hii baadae unapata wafuasi wengi na unatengeneza kipato kitakachokuwezesha kuacha kazi kabisa na kufanyia kazi zako nyumbani au popote unapochagua.

  Unahitaji nini ili kufikia kiwango hiki?

Ili uweze kupata mbinu bora za kutengeneza pesa kupitia mtandao unahitaji elimu na ujuzi muhimu kuhusiana na biashara hii ya kutumia mtandao.

  Kutokana na umuhimu wa elimu hii nimeandaa kozi fupi kwa wale wote ambao wanahitaji kutengeneza kipato kupitia mtandao. Kozi hii itafundishwa kwa siku kumi na itafundishwa kwa njia ya mtandao hivyo utaweza kuifuatilia popote ulipo duniani.

  Katika kozi hii utajifunza vifuatavyo;

1. Utambulisho wa blog na aina mbalimbali za blog.

2. Njia mbalimbali za kutengeneza fedha kupitia blog.

3. Kuweka misingi ya blog yako na kuchagua mtindo wako.

4. Uandishi wa makala zenye mvuto.

5. Kujenga hadhira na kuvutia wasomaji wengi zaidi(email list).

6. Kuunganisha blog na mitandao mingine ya kijamii ili kupata wasomaji wengi zaidi.

7. Kuchagua njia ya kuingiza fedha kutumia blog.

8. Uandishi wa makala za kuuzia bidhaa au huduma na siri iliyoko nyuma ya utafutaji wa masoko.

9. Kutengeneza fedha kusiko na kikomo kupitia blog yako.

10. Kutofautisha blog yako na blog nyingine na jinsi ya kuendelea kuikuza zaidi.

  Kozi hii itafundishwa kwa njia ya mtandao na itachukua muda wa siku kumi tu. Gharama ya kozi hii ni shilingi elfu kumi za kitanzania.

  Kujiunga na kozi hii tuma fedha(tsh 10,000/=) na email yako kwa mpesa au tigo pesa 0755953887/0717396253 kisha utaingia kwenye kozi hii. Kozi itaanza rasmi tarehe 28/04/2014. Mwisho wa kujiunga na kozi hii ni ijumaa ya wiki hii tarehe 25/04/2014.

  Wahi kujiunga na kozi hii kabla muda haujaisha. Hatutapokea watu baada ya muda wa kulipa kupita au katikati ya kozi.

  Hii ni nafasi kubwa sana kwako kuweza kutengeneza kipato cha uhakika na kisicho na kikomo. Dunia inabadilika kwa kasi sana na mtandao wa internet umetengeneza matajiri wengi sana duniani. Usiachwe nyuma na njia hii ya kipekee na ya uhuru ya kujiingizia kipato.

  Karibu kwenye ukombozi wa maisha yako kiuchumi.

2 thoughts on “Dunia Inabadilika Kwa Kasi Sana, Fanya Hivi Ili Usipitwe Na Mabadiliko Haya.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: