Kama ulivyo utaratibu wa mtandao wa AMKA MTANZANIA kila mwezi wewe msomaji unatumiwa kitabu kizuri cha kujisomea. Kitabu hicho kinakuwa na mbinu mbalimbali za kuweza kukusaidia kuvuka changamoto unazokutana nazo au kutumia fursa zinazokuzunguka ili kufikia mafanikio makubwa kimaisha.
Vitabu unavyotumiwa ni vitabu ambavyo watu wengi duniani wamekiri kubadilisha maisha yao kwa kusoma vitabu vya aina hii. Hivyo na wewe msomaji kama unasoma vitabu hivi ni lazima maisha yako yatabadilika na kuwa bora zaidi, ILA TU KAMA UTACHUKUA HATUA YA KUFANYA YALE UNAYOJIFUNZA.
Mwezi huu wa tano nakutumia kitabu THE SCIENCE OF GETTING RICH kilichoandikwa na WALLES D. WATTLES.
Hivi unajua kwamba kuna sayansi ya kupata utajiri? Huenda hujui hilo, na sio kosa lako kwa sababu hakuna sehemu yoyote kwenye mfumo wa elimu au kwenye maisha ya kijamii unafundishwa sayansi hii. Unashangaa kwa nini umesoma, unafanyakazi kwa bidii, umeanzisha na biashara ila bado hufikii utajiri unaotazamia? Unashangaa kwa nini kuna watu wanaonekana ni wa kawaida sana ila wanapata mafanikio makubwa sana kifedha kuliko wewe? Kuna sayansi ya utajiri ambayo mpaka sasa wewe hujaijua.
Watu wachache sana wanajua sayansi hii ya kupata utajiri ila pia hawapo tayari kuwafunsisha wengine ndio maana jamii imejaa watu wengi ambao wanahangaika kupata utajiri ila hawaupati.
Sayansi hii sio ya kufanya maabara au kutumia nguvu za miujiza, bali ni mambo ambayo unaweza kuanza kufanya leo na maisha yako yakabadilika kwa kiwango kikubwa sana.
Kupitia kitabu hiki utajifunza njia mbalimbali za kutengeneza na kuendeleza utajiri wako. Kupitia kitabu hiki utajifunza mbinu ambazo kama ukizitumia utajiri utakufuata wewe badala ya wewe kuukimbiza na kuishia kuchoka bila kuupata.
Kuna vitu vingi sana vya kujifunza kwenye kitabu hiki. Nakushauri sana ukisome kitabu hili.
Kwa wale wavivu wa kusoma najua umeshaanza kusema huna muda wa kukisoma. Sasa ngoja kwa kifupi sana nikuoneshe ni jinsi gani unaweza kukisoma kitabu hiki bila ya kutumia nguvu au kubadili ratiba zako.
Kitabu hiki kina kurasa 64, ila kurasa zenye maandishi unayotakiwa kusoma ni 51. Kwa kurasa hizi 51 kama umepanga kuzisoma ndani ya mwezi mmoja(siku30) ina maana kwa siku soma kurasa mbili tu ambazo hazitakuchukua hata dakika tano. Kwa mpango huu utajifunza mambo mengi sana.
Kitabu hiki kimetumwa kwa wanachama wa mtandao wa AMKA MTANZANIA. Kama unataka kupata kitabu hiki na bado hujawa mwanachama wa AMKA MTANZANIA bonyeza maandishi haya na uweke email yako, baada ya kukamilisha kujiunga utatumiwa email yenye link ya kitabu hiki. Bonyeza link hiyo na utaanza kudownload kitabu hiki mara moja.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa. Kumbuka hakuna kitu chochote au mtu yeyote anayeweza kukuzuia kufikia mafanikio makubwa unayotazamia, ni wewe mwenyewe tu.
TUKO PAMOJA KWENYE SAFARI HII.