Kwa miaka mingi sasa umekuwa dalali wa maisha yako na umeweza kuyadalalia vizuri sana. Japo unayadalalia maisha yako hujajua kuwa unafanya hivyo. Hii inatokana na kwamba wewe unaamini unachofanya ndio sahihi. Unaweza kuona ni sahihi lakini ukifikiri kwa kina utaona sio sahihi kwa sababu kila siku maisha yako yanazidi kuwa magumu.

muda na pesa

Unafanyaje udalali wa maisha yako?

Kila siku za wiki duniani kati ya saa kumi na moja mpaka saa kumi na mbili na nusu asubuhi alamu nyingi sana zinaita. Alamu yako ni moja wapo, inaita, unaizima na kusema ujipe dakika tano za kumalizia usingizi wako. Unashtuka nusu saa baadae, umeshachelewa, unajiandaa haraka haraka unakosa hata muda wa kupata kifungua kinywa. Unatoka nyumbani kuelekea kazini unakaribishwa na foleni, unakaa kwenye foleni hii kwa zaidi ya saa moja, wakati mwingine mawili ndio uweze kufika kazini. Unafika kazini wakati mwingine umechelewa kidogo unaingia na kuanza kujiweka bize na kazi zako. Wakati mwingine hakuna kazi kubwa unayofanya ila unajitahidi kuwa bize bize ili uonekane kuna kazi kubwa unafanya.

Muda wa chai unafika, unaenda kunywa chai, unatafuta muda kidogo wa kupoteza poteza na unachelewa kurudi. Ukirudi kwenye kazi unaendelea na kazi kidogo, unaingia kwenye mtandao nako unaendelea kupoteza muda kidogo. Muda wa kula unafika, unakwenda kula unapiga soga kidogo na wenzako, unarudi tena kwenye kazi yako kujiandaa kuondoka. Saa tisa na nusu inafika unaona kama muda hauendi ili kufika saa kumi au saa kumi na moja na uondoke.

Hatimaye muda wa kuondoka unafika, unafurahia kidogo na kuondoka. Unaingia tena kwenye foleni itakayochukua zaidi ya masaa mawili. Unafika nyumbani au sehemu uliyozoea kupumzika, labda unapata moja moto na moja baridi. Unarudi nyumbani unafanya kazi zako kidogo kisha unakwenda kukaa mbele ya kompyuta au tv na kuangalia mambo yasiyo na mchango kwenye maisha yako kwa zaidi ya masaa mawili. Unachelewa kulala na kesho alamu inaita tena na mzunguko woote unajirudia.

Unarudia mzunguko huo kila siku mpaka inapofika tarehe ishirini na nane(au ishirini na sita au thelathini kwa wengine). Unaenda kwenye ATM na kuona salio limeogezeka, mshahara umeingia, unakuwa na furaha sana. Lakini furaha hii haitamaliza siku moja kwa sababu una madeni mengi ya kulipa, una vitu vingi vya kununua na kuna majambazi wa hiari wanakunyemelea nao wapate sehemu hiyo ya mshahara wako.

Baada ya kulipa madeni unayodaiwa na kununua mahitaji ya msingi chenchi ndogo iliyobaki unashawishika kuipeleka kwenye vitu ambavyo havina msaada kabisa kwenye maisha yako(majambazi wa hiari). Kwa mfano mwisho wa mwezi ndio baa nyingi zinajaa na ndio watu mbalimbali wanaandaa matamasha ya burudani. Yote haya ni kunyemelea chenchi yako iliyobaki.

Baada ya siku mbili unarudia mzunguko wako, unaanza tena kukopa na kuhesabu siku mpaka kufikia tarehe ishirini na nane.

Unafanya hivi mwaka wa kwanza, wa pili, wa kumi na baadae kazi inaisha huku hujajipanga kwa lolote.

Hivi ndivyo unavyodalalia maisha yako, unatoa muda wako kufanya kazi ili upate fedha halafu unachukua fedha hiyo na kuwapelekea wengine huku wewe ukibaki mikono wazi! Hebu niambie maisha yako yana thamani gani kwa njia hii? Yaani hujawahi kuwa na uhuru wa muda wako wala fedha yako? Vyote umeweka rehani wenye kuweza wavitumie, aliekuajiri anatumia muda wako, matumizi yanatumia fedha zako, unabaki bila ya chochote.

Leo nakuambia hii sio sahihi kabisa kwenye maisha yako. Umeyadhulumu maisha yako kiasi cha kutosha sasa.

Leo nataka uchukue nafasi ya kujifunza jinsi ya kuacha udalali huu wa maisha yako. Uanze kuwa na umiliki wa vitu hivi viwili muhimu kwenye maisha yako, muda na fedha.

Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA mwezi wa tano tulijifunza jinsi ya kuweza kutumia muda vizuri ili kuweza kuongeza kipato chako hata kama umeajiriwa. Na mwezi huu wa saba tutajifunza jinsi ya kutunza na kutumia fedha zako ili kuweza kuondoka kwenye utumwa uliopo sasa.

Kujifunza mambo haya muhimu sana kwenye maisha yako jiunge na KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kuboresha maisha yako.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA jiunge mapema kabla ya mwezi huu kuisha. Kujiunga tuma fedha tsh elfu kumi(10,000/=) kwa mpesa 0755953887 au tigo pesa 0717396253 kisha utume email yako(email ya GMAIL ni bora zaidi) na utaunganishwa.

Mwisho wa kujiunga ni jumatatu, fanya hima usipoteze nafasi hii muhimu kwenye maisha yako.

Nakutakia kila la kheri kwenye safari ya kuboresha maisha yako.

TUKO PAMOJA.

kitabu kava tangazo