Katika makala ya uwekezaji kwa watu ambao hawana muda tulizungumzia aina mbalimbali ambazo mtu ambaye hana muda wa kufuatiliasana uwekezaji wake anaweza kuzifanya. Moja ya aina hizo za uwekezaji ni ununuaji wa hisa na ununuaji wa vipande.
Leo hapa tutajadili ununuaji wa vipande na tutatumia vipande vya Mfuko wa Umoja(UNITY TRUST OF TANZANIA).
UTT ni mfuko ambao umepewa dhamana ya kukusanya mitaji na kuwekeza sehemu mbalimbali. Katika kukusanya huko mtaji wametengeneza mfumo ambao mtu yeyote anayetaka kuwekeza anaweza kufanya hivyo bila ya kujali ana fedha kiasi gani.
Na ili kuweza kuwapatia watu wote fursa, UTT wametengeneza vipande ambapo kipande kimoja kina thamani ndogo ambayo kila mtu anaweza kuimudu. Kwa mfano kwa tarehe ya leo kipande kimoja kinauzwa tsh 438. Hivyo mtu yeyote anaweza kununua vipande hivi na kiwango cha chini ni kununua vipande vya tsh elfu kumi.
Vipande vinafanyaje kazi?
Kwanza vipande hivi sio kwamba ni vikaratasi unapewa bali ni thamani tu ya fedha zako. Sasa tunavyolipia thamani hii wao UTT wanakusanya fedha hizo na kwenda kuwekeza kwenye makampuni mbalimbali ambayo yanafanya vizuri kwenye biashara. Kwa kuwekeza huko wao wanapata gawio na gawio hilo hulileta kwako wewe unayemiliki vipande. Hii imerahisisha sana kwa watu wenye mitaji kidogo kuweza kuwekeza kwenye biashara kubwa.
Wewe unanufaikaje?
Kama tulivyoona hapo juu UTT wao wakwenda kuwekeza kwenye biashara kubwa, faida wanayoipata kule wanaileta na kuiongeza kwenye thamani ya vipande. Hivyo faida utakayoipata wewe ni vipande vyako kuongezeka thamani. Kwa mfano wakati mimi naanza kununua vipande, kipande kimoja kilikuwa tsh 350, leo hii thamani ya kipande kimoja ni tsh 438, hii ina maana kwamba kama ningekuwa nnimenunua vipande elfu kumi kipindi hiko ambayo ingekuwa ni tsh mil 3.5 ningeamua kuviuza leo ningepata mil 4.3, Ni fedha nyingi ila inahitaji muda pia.
Kwa hiyo kila siku thamani ya vipande inaongezeka kulingana na uchumi na biashara pia. Kama unataka kupata fedha yako unauza vipande vyako na unapewa fedha kulingana na bei ya vipande siku hiyo unayouza.
Na kwenye kuuza vipande sio kwamba wewe ndio unatafuta soko, hapana, unajaz afomu ya kuuza vipande na ndani ya siku kumi unapewa fedha zako.
Jinsi ya kuanza kuwekeza na UTT.
Ili kuanza kununua vipande na kuwekeza unakwenda kwenye ofisi zao na kujaza fomu kisha unapewa namba yako. Kununua vipande unaweza kulipia kwa CRDB au kulipia kwa MPESA. Na hapa mimi ndio ninapopapenda kwa sababu unaweza kulipia kwa mpesa ukiwa popote. Ukiwa mwanachama utaelekezwa utaratibu huo wa MPESA na hivyo kuwa rahisi sana kwako kuwekeza.
Kwa walioko dar unaweza kutembelea ofisi zao ambazo zipo SUKARI HOUSE barabara ya sokoine. Kwa walioko mikoani unaweza kuwasiliana nao ili kujua utaratibu. Mawasiliano yanapatikana kwenye tovuti yao ambayo ni http://www.utt-tz.org
Ushauri wangu.
Nashauri mtu yeyote ambaye anaweka fedha benk afikirie kuwekeza kwenye vipande hivi. Japo faida yake sio kubwa sana ila ni afadhali ukilinganisha na benki ambapo unapewa riba chini ya asilimia moja. UTT wanakuhakikishia kwamba kwa mwaka unapata asilimia kumi ya kile ulichokiweka, ila inaweza kuwa zaidi ya hapo. Kwa mfano wanasema kwa mwaka jana waliowekeza walipata asilimia 48, yaani kama mtu alikuwa amewekeza milioni kumi alipata riba ya milioni 4.8, hii ni faida kubwa sana ambayo huwezi kuipata kwenye biashara yoyote.
Hivyo kwa wale ambao wanakusanya fedha kwa ajili ya kupata mtaji hii pia ni sehemu nzuri sana ya kufanya hivyo.
ANGALIZO; Kama unataka aina hii ya uwekezaji iwe ndio uwekezaji mkubwa kwako inabidi uwe na uvumilivu na usiwe na haraka maana jinsi muda unavyokwenda ndivyo uwekezaji wako unavyoongezeka thamani. Kwa mfano wanasema mwaka 2005 kipande kimoja kilikuwa kinauzwa tsh 70 hivyo kama mtu alinunua vipande laki moja kwa gharama ya tsh milioni 7 leo angekuwa na thamani ya milioni 43.8 hapo hajafanya kazi yoyote na wala hajaongeza chochote.
UTT wana mifuko mingi sana, hapa nimezungumzia mfuko mmoja wa umoja ambao mimi ndio nawekeza humo. Kuna mifuko mingine kama WATOTO, JIKIMU, WEKEZA MAISHA.
Kupata maelezo zaidi kuhusu UTT BONYEZA HAPA na uingie kwenye tovuti yao.
Kupata maelezo ya bei za vipande kwa siku husika bonyeza hapa.
Nakutakia kila la kheri katika kuendelea kutafuta fursa za uwekezaji.
TUKO PAMOJA.
kaka hakika katika utoaji Wa fungu LA kumi kiroho safi umewazid wengi.kwa elimu Hii pepo utaiona Mkuu.si unajua tunaangamia kwa kukosa maarfa.
LikeLike
Ni kweli kabisa kaka,
Kukosekana kwa maarifa ndio chanzo cha matatizo makubwa yanayowapata watu.
Asante sana kaka,
TUKO PAMOJA.
LikeLike
“…UTT wanakuhakikishia kwamba kwa mwaka unapata asilimia kumi ya kile ulichokiweka, ila inaweza kuwa zaidi ya hapo. Kwa mfano wanasema kwa mwaka jana waliowekeza walipata asilimia 48, yaani kama mtu alikuwa amewekeza milioni kumi alipata riba ya milioni 4.8, hii ni faida kubwa sana ambayo huwezi kuipata kwenye biashara yoyote.”
Makirita, kwa mujibu wa nukuu hapo juu, ina maana UTT wanatoa gawiwo la pesa (dividend)kila ifikapo mwisho wa mwaka? Naomba nisikie toka kwako kabla sijawatafuta wenyewe.
LikeLike
Habari Dotto,
UTT hawatoi gawio bali thamani ya vipande vyako inakua. Kwa mfano umenunua kipande kwaka jana na bei yake ilikuwa shilingi mia tatu, mwaka huu kipando hiko kikawa kipemanda thamani mpaka kufikia 450 ina maana kama ulinunua vipande vya shilingi milioni tatu ukiuza mwaka huu unapata milioni nne na nusu. Ndio hivyo unavyofaidika na thamani hiyo.
LikeLike
Ahsante sana Kocha kwa Somo,
Hapa nachukua hatua kujua mikoani nawapataje.
LikeLike
Sawa,
Vizuri sana.
LikeLike