It is not what you do for your children, but what you have
taught them to do for themselves, that will make them successful human beings.
–Ann Landers

Sio kile unachowafanyia wanao ndio muhimu, bali kile
ulichowafundisha kufanya kwa ajili ya maisha yao ndio kitawafanya
wafanikiwe.

Umekuwa ni utamaduni wa wazazi kutaka kuwafanyia watoto wao kila
kitu ili wawe na maisha bora. Ila pale wazazi wanapoondoka watoto hawa wamekuwa
wanapata shida sana.

Ni muhimu kuwafundisha watoto jinsi ya kutengeneza maisha yao
wenyewe badala ya wewe mzazi kujaribu kuwajengea maisha, hutawasiadia kwa
kuwajengea maisha yao.

Nakutakia siku njema.