Mpendwa msomaji wa AMKA MTANZANIA kwama tulivyotangaza awali, AMKA CONSULTANTS imeandaa semina ya siku 21 itakayofanyika kwa njia ya mtandao. Mafunzo ya semina hii yatatolewa kwa siku 21 na yatatumwa kwa njia ya email.

Semina hii imelenga kukuandaa wewe msomaji ili kuweza kufanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yako kwa mwaka 2015. Baadhi ya mambo utakayojifunza kwenye semina hii ni;

1. Kufungua uwezo mkubwa ulioko ndani yako.

2. Kubadili maisha yako.

3. Kutengeneza maisha yako ya baadae.

4. Kujua thamani ya maisha yako na vile unavyovithamini.

5. Kujua malengo yako ya kweli.

6. Kujua dhumuni lako kubwa kwenye maisha.

7. Jinsi ya kuvuka vikwazo unavyokutana navyo.

8. Jinsi ya kubobea kwenye kile unachofanya

9. Jinsi ya kutumia muda wako vizuri.

10. Jinsi ya kufikia ubunifu mkubwa uliopo ndani yako.

11. Jinsi ya kujijengea uvumilivu ili kuweza kufikia malengo yako.

Haya na mengine mengi utapata nafasi ya kujifunza kwenye semina hiyo itakayofanyika kwa siku 21. Semina itaanza tarehe 05/01/2015.

Ili kujiunga na semina hii unahitaji kulipa ada ambayo ni tsh elfu kumi kwa tigo pesa/airtel money 0717396253 au mpesa 0755953887 na kisha kutuma jina na email yako kwenye moja ya namba hizo.

Mwisho wa kujiunga na semina hii ni leo tarehe 31/12/2014, ikishapita hutapata tena nafasi ya kujiunga na semina hii. Na kwa bahati mbaya sana semina hii haitarudiwa tena kwa mwaka 2015, hivyo unayo nafasi ya leo ili kujihakikishia mafunzo ya semina hii.

Ni muhimu sana wewe kupata mafunzo haya kwa sababu yatakuwa msaada mkubwa kwa wewe kubadilika.

Ni nini kinakufanya mpaka sasa hujajiunga?

Nafikiri hivi ni baadhi ya vitu ambavyo vinakufanya usione umuhimu wa kujiunga mpaka sasa.

1. Sina hiyo elfu Kumi ya kujiunga.

Ndugu kama kwa mwaka mzima 2014 hujaweza kutengeneza elfu kumi ya ziada ambayo utaweza kulipia mafunzo ya kukuendeleza basi upo kwenye hatari kubwa. Na wewe ndio muhimu sana kupata mafunzo haya ili mwaka 2015 usiendelee kuwa na matatizo hayo ya fedha, maana utakapobadili maisha yako na hata kiwango cha fedha unachopata kitaongezeka. Fanya chochote unachoweza kufanya hata kama ni kukopa au kuomba upate hiyo elfu kumi ili upate mafunzo haya.

2. Nimeshasoma sana mambo haya hivyo hakuna jipya.

Kama hiki ndio unachofikiria na kinakufanya uone sio muhimu kujiunga na semina hii upo kwenye njia ya kupotea. Kujifunza hakuna kikomo, hakuna siku ambayo utasema nimeshajua kila kitu, na ukifikia kusema hivyo ndio unaanza kuporomoka. Hivyo tumia kila nafasi ya kujifunza unayoipata, kuna kitu kipya cha kujifunza kila siku.

3. Naogopa kutapeliwa kwenye mtandao.

Kama kinachokufanya ushindwe kujiunga ni kuogopa kutapeliwa fedha yako kwenye mtandao hii ina maana wewe ni msomaji mpya kwenye AMKA MTANZANIA. Kwa sababu wasomaji wa kila siku wanajua jinsi ambavyo tumekuwa tukitoa mafunzo na huduma nyingine nyingi kwa njia ya mtandao. Hivyo unaweza kuamua kutokuchukua nafasi ili kuepuka kupoteza fedha yako, au ukasoma makala hizi kumi zilizosomwa sana mwaka 2014 na kisha ujiulize kwa makala hizo kuna mtu atapanga kukuibia wewe shilingi elfu kumi. Fanya hivyo haraka ili upate nafasi ya kulipia ada na uweze kupata mafunzo haya mazuri.

Kwa hayo machache naomba nikushauri ufanye hima kupata nafasi yako leo. Kama katika sikukuu hizi ulivaa vizuri, ukala vizuri na kunywa vizuri ni wakati sasa wa kuipendezesha akili yako kwa kuilisha chakula kizuri na kuifanya iweze kukuletea mambo makubwa mwaka 2015.

Kumbuka leo ndio mwisho wa wewe kupata nafasi ya kujinga na mafunzo haya na mafunzo yataanza tarehe 05. Tuma ada ya mafunzo sasa(tsh elfu kumi) pamoja na jina na email yako kwenye namba 0717396253/0755953887.

Nakutakia kila la kheri kwa masaa machache yaliyobakia kumaliza mwaka 2014 na maandalizi mema ya mwaka 2015.

TUPO PAMOJA.