There is far more opportunity than there is ability. -Thomas A. Edison

Kuna fursa nyingi sana kuliko uwezo wa watu kuzitumia fursa hizo.

Usidanganyike kwamba hakuna fursa, fursa zipo nyingi sana. Kama mpaka sasa hivi huzioni fursa maana yake uwezo wako bado uko chini kuliko fursa zinazokuzunguka. Kama utaongeza uwezo wako utaanza kuona fursa nyingi ambazo umekuwa unazipita kila siku. SOMA; NENO LA LEO; Kama Bado Hujaipata Fursa Fanya Hivi… Badala ya kujiuliza nitapata wapi fursa, jiulize je nina uwezo wa kutambua na kuzitumia fursa? Kama jibu ni hapana jijengee uwezo, anza kujifunza sasa na kutanua uwezo wako na baadae utaona mabadiliko makubwa. Ujifunzie wapi? Kama mpaka sasa hujajua basi ingia maeneo haya na ujifunze zaidi; AMKA MTANZANIA KISIMA CHA MAARIFA JIONGEZE UFAHAMU  MAKIRITA AMANI  Nakutakia siku njema. SOMA; NENO LA LEO; Jinsi Ya Kupata Fursa Bora.