Kama utajifunza biashara kabla ya kuingia kwenye biashara utajifunza vitu vingi sana. Utajua kila aina ya kanuni na kila aina ya mbinu ya kuanza na kukuza biashara yako.
Lakini unapoingia kwenye biashara yenyewe mambo hayaendi kiulaini kama ulivyokuwa unajifunza. Kwenye biashara halisi sio kwmaba kila kitu kitakwenda kama ulivyokuwa umepanga kabla ya kuanza.
SOMA; Faida kumi za kuwa na MAONO kama nilivyojifunza kwenye kitabu THE PRINCIPLES AND POWER OF VISION.
Kama ulikuwa umeandaa mchanganuo wa biashara yako, sio mambo yote yatakwenda kama ulivyokuwa umepanga.
Kwa kifupi ni kwamba utashindwa mara kadhaa kwenye biashara yako. Na hapa ndio pazuri sana maana unajifunza mambo mengi sana kwenye kushindwa kuliko yale unayojifunza kwa kujisomea au kwa kufanikiwa.
SOMA; Huu Ndio Mtaji Mkubwa Ambao Tayari Unao.
Unaposhindwa maana yake unajua ni njia ipi haifai na hivyo kuiepuka wakati mwingine.
Kushindwa kwenye biashara maana yake ni kukua. Unapokutana na changamoto itakufanya ufikiri zaidi ya kikomo ulichojiwekea. Ni katika kufikiri huku ndio unakua zaidi na kuweza kufikia ngazi za juu kwenye biashara yako.
Usiogope kushindwa, usiumie sana unaposhindwa. Jua kushindwa hasa mwanzoni ni moja ya masomo ya biashara na jiandae ili kuweza kuvuka changamoto za aina hii. Hakuna kitakachokushinda kama utaamua kutokushindwa.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.