Ndio akili ya mteja inavyowaza hivi hata kama hakuambii.

Biashara za kupiga kelele sasa hivi zimeshapitwa na wakati. Hizi ni zama za biashara za kutoa sababu. Tuambie kwa nini tufanye biashara na wewe.

Kupiga kelele.

Kupiga kelele ni pale ambapo unatumia nguvu nyingi kutangaza biashara yako, ila unashindwa kujenga mahusiano na mteja. Hapa ni pale unapotangaza kwamba kampuni yako ni bora sana na inaweza kufanya hiki na kile na kile. Kwa bahati mbaya sana mteja hahitaji kujua kampuni yako ina ukubwa kiasi gani, wala hataki kujua ina ubora kiasi gani, kuna kitu kimoja anataka kukisikia, na kwa bahati mbaya hakipo kwenye kelele unazopiga.

SOMA; Usiweke Maanani Unachoambiwa Na Mtu Aliye Kwenye Hali Hizi Tatu.

Kutoa sababu.

Hii ndio njia mpya ya kutangaza biashara yako, hata kama huitangazi. Hapa ni pale unapompa mteja sababu ya kufanya biashara na wewe. Hapa unampa lile neno ambalo anataka kulisikia, unajibu swali lake kwa nini afanye biashara na wewe. Unamwambia ni jinsi gani biashara yako itatatua matatizo yake. Na atafurahi sana kufanya biashara na wewe hasa pale utakapofanikiwa kutatua matatizo yake.

SOMA; BIASHARA LEO; Biashara Yako Ni Matatizo Ya Watu…

Usipige kelele, kila mtu anaweza kufanya hivyo. Toa sababu, na watu wataifuata sababu hiyo.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.