Pamoja na uwezo mkubwa ambao tunao, pamoja na maarifa mengi tunayoweza kujikusanyia bado hakuna mtu anayeweza kuitabiri kesho kwa asilimia 100. Hakuna.
Hakuna anayejua ni nini kitakachotokea kesho kwenye maisha yake au biashara yake. Lakini hii haituzii kuweka na kufanyia kazi mipango yetu kwenye maisha na biashara zetu.
SOMA; Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.
Kwa kuwa hatuna uhakika na kesho yetu, mara nyingi sana tumekuwa tunaweka mipango lakini tunashindwa kuitekeleza kwa wakati. Tunajua kabisa ni kitu gani tunataka na tunakiwekea mipango mizuri lakini tunashindwa kukifikia. Mara nyingi hali hii huwaumiza watu wengi na wengine huchukulia kama wameshindwa au hawawezi biashara.
Leo nataka nikuambie usiumie tena na hali hii, haitokei kwako mwenyewe na huwezi kuthibiti kesho yako. Unaweka mipango leo lakini hujui nini kitatokea kesho. Hivyo kujilaumu hakuwezi kukusaidia. leo nakushiriksiha sheria koja muhimu itakayokuwezesha kuondokana na hali hii ya kushindwa kufikia maipango yako kwa wakati.
SOMA; USHAURI; Kabla Hujachukua Mkopo Ondokana Na Tabia Hii Kwanza.
Sheria hii inaitwa MARA MBILI, MARA TATU. Sheria hii ina maana kwamba katika mipango yako yote ya fedha weka MARA MBILI. Kwa mfano kama umesema biashara unaotaka kufanya unahitaji shilingi milioni 10 basi tafuta milioni 20. Hii ni kwa sababu kwamba mahitaji yako ya fedha yatakuw amakubwa kuliko ulivyopanga. Pia katika mpango wa muda fanya MARA TATU. Kama unafikiri bashara yako itakuwa imesimama baada ya miezi miwili weka miezi sita. Kama unafikiri mzigo ulioagira utafika ndani ya siku moja weka siku 3. Hii itakuondolea usumbufu pale jambo linaposhindwa kukamilika kwa wakati.
Sio mara zote utahitaji fedha mara mbili na sio wakati wote muda utakuwa mara tatu. Ila tuna uhakika kwamba utahitaji fedha zaidi ya ulizapanga sasa na utahitaji muda zaidi ya uliotenga sasa. kwa kujiwekea nafasi kubwa ya fedha na muda kunakufanya ufanye biashara yako kwa uhuru sana na kuepuka kuwa na msongo wa mawazo kila mara ambapo mambo hayajakwenda kama ulivyopanga.
SOMA; Mteja Hajui Anachotaka, Ila Anajua Kitu Hiki Muhimu Sana.
Biashara yenyewe tu tayari ni ngumu, usitake kuongeza ugumu wake kwa mipango yako mwenyewe. Iweke mipango yako kwa nafasi ya kukutosha wewe kuifanya kwa ufanisi na ukiw aumetulia.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.