Moja ya changamoto ambazo zinawazuia wafanyabiashara wengi kufikia mafanikio ni upatikanaji wa wateja.
Wafanyabiashara wengi sana hutumia nguvu nyingi kumfanya mteja afike kwenye biashara yake, lakini mteja anapofika pale anajilaumu ni kitu gani kimempeleka pale na hatokuwa tayari kurudi tena.
SOMA; Maswali Matatu Muhimu Ya Kujiuliza Kwenye Wazo Lako La Biashara.
Mtu anakazana kutangaza kwa njia mbalimbali na kufanikiwa kumfikisha mteja wkenye biashara yake, ila huduma anayokwenda kuipata mteja hamshawishi kabisa kurudi tena kwenye baishara hiyo.
Leo nakuambia wateja rahisi sana kuwapata kwenye biashara yako ni wale ambao umeshafanya nao biashara. Hii ina maana kwamba kama mtu ameshafanya baishara na wewe huyo ndio mteja rahisi kumpata tena na tena na tena. Ila hutampata kwa sababu tu ameshafanya biashara na wewe, utampata kama utafanya juhudi za kumpata tena.
Na juhudi hizi ni kutoa huduma iliyo bora sana kwa mteja wako. Kuhakikisha unayafikia na kuyapita matarajio yake. Na kuhakiksiha mteja huyu anakuwa shabiki wako namba moja na anakuwa tayari kuwaambia wengine kuhusiana na biashara yako.
SOMA; Kitu Muhimu Kujua Kuhusu Mteja Wako.
Usiache mteja huyu rahisi kupatikana aondoke wakati wewe unakazana kuita wengine ambao nao wataondoka. Kuwa na mkakati madhubuti wa kuhakikisha kila mteja anayefika atarudi tena na tena na tena.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.