Sote tunajia kwamba biashara zina changamoto nyingi sana. Na sehemu kubwa ya changamoto hizi huwa tunazitengeneza sisi wenyewe kwa kufanya au kutokufanya mambo fulani. Na kila changamoto tunayokutana nayo kwenye biashara tunaweza kuitatua kama tukijua njia sahihi za kuikabli changamoto husika. Kupitia kipengele hiki cha BIASHARA LEO hapa kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunashirikishana mbinu mbalimbali za kuwez akutatua changamoto za kibiashara tunazokutana nazo.
Leo tutaangalia kosa kubwa sana ambalo unaweza kulifanya wkenye biashara yako na likakugharimu sana. Kosa hili limekuwa linafanywa na wafanyabiashara wengi ambao wamefikia mafanikio kiasi na limekuwa linachangia sana kwenye kuanguka kwao kibiashara.
SOMA; Hivi Ndio Vitu Vinavyopelekea Ongezeko La Thamani Ya Hisa Kwa Mwekezaji.
Kosa hili ni KURIDHIKA na kuona umeshaweza kila kitu. Katika ulimwengu wa sasa ambao mabadiliko yanatokea kwa kasi sana, hakuna mtu anayeweza kusema wkamba yeye ameshapatia au ameshajua kila kitu. Kila siku mambo yanabadilika, kila siku kuna kitu kipya cha kujifunza, kila siku kuna mbinu mpya za kujaribu. Ukishajiona kwamba wewe upo juu na hivi vingine vyote havijali, jua umeanza safari yako ya kuporomoka.
Kila wakati kwenye biashara yako, iwe ndio unaanza au una miaka 20 kwenye biashara, kuwa tayari kujifunza, kuwa tayari kujaribu mambo mapya na kuwa tayari kubadilika ndio kitu pekee kitakachokuwezesha kuendelea kuwepo kwenye ulimwengu wa sasa wa biashara. Ukiridhika na kuona wewe umeshafikia kiwango cha juu sana na hivyo huna haja ya kujifunza tena au huna haja ya kubadilika, kumbuka kuna vijana wana kiu kubwa ya mafanikio na wanafanya kazi usiku na mchana kukuondoa wewe kwenye biashara uliyopo. Wanaweza kuwa hawafanyi kazi ya kukuondoa wewe moja kwa moja ila kile wanachokifanya kinapofanikiwa wewe unapotezwa.
SOMA; Usikazane Kushindana, Kazana Kuwa Bora.
Naposema usiridhike sina maana kwamba ujione kwamba hujafanya chochote, ila jione kwamba bado una safari ndefu ya kwenda. Sio kwamba siku moja utafika mahali ndio ufurahie mafanikio, bali safari yenyewe ndio ya kufurahia.
Endelea kujifunza, endelea kujiuliza maswali na endelea kujaribu njia mpya za kibiashara. Pia usikose semina ya MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015 ambapo utajifunza mbinu mbalimbali za kuanza, kukuza na kufikia mafanikio makubwa kwenye biashara yako. Kwa maelezo zaidi soma; Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.
AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.