Leo Ndio Siku Ya Mwisho Ya Kujiunga Na Semina Ya Mafanikio Kupitia Biashara.

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA? Naamini upo vizuri na unaendelea na shughuli zako mbalimbali ili kuweza kufikia malengo na mipango uliyojiwekea kwenye maisha yako. Hongera sana kwa kuuanza mwezi mpya wa tano. Siku zinakwenda, ni juzi tu tumeuanza mwaka ila muda sio mrefu tunakaribia kufikia nusu ya mwaka. Je kwa muda unavyokwenda na wewe unavyoendelea unaona utaweza kuyafikia malengo uliyojiwekea kwa mwaka huu 2015? Hili ni swali muhimu kujiuliza kila siku.

Leo tarehe 01/05/2015 ndio siku ya mwisho ya wewe kuweza kujiunga na semina ya MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA. Hii ni semina iliyoandaliwa na AMKA CONSULTANTS kwa ajili ya kutoa maarifa kwa wafanyabiashara wanaoanza na wale ambao ni wazoefu kuweza kukuza biashara zao na kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Kila mmoja wetu anajua jinsi gani nyakati hizi zilivyo na changamoto nyingi. Hata kama mtu una mafanikio kiasi gani kwenye biashara, bado kuna changamoto mpya zinazoibuka kila siku na zinazoweza kukuondoa kabisa kwenye biashara hiyo.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao na masomo yatatumwa kwa njia ya email kila siku asubuhi kwa muda wa mwezi mmoja. Mshiriki atasoma somo husika na kama atakuwa na swali lolote anaweza kuuliza kwa kujibu email hiyo na akapatiwa majibu ya swali lake.

Semina itaanza jumatatu tarehe 04/05/2015. Ada ya semina hii ni tsh elfu 30. Kupata nafasi ya kushiriki tuma ada hiyo kwneye namba 0717396253 au 0755953887 na kisha tuma ujumbe wenye jina lako na email yako na utaandikishwa kwenye masomo haya. MWISHO WA KUJIUNGA NA SEMINA HII NI LEO TAREHE 01/05/205 hivyo kama hutaki kukosa masomo haya hakikisha unatuma ada hiyo kabla ya siku ya leo kuisha.

Kwa kushiriki sekina hii utajifunza mbinu mbalimbali za kukuwezesha kukuza biashara yako zaidi na kufikia mafanikio makubwa. Baada ya mafunzo haya hutobaki kama ulivyokuwa awali. Kuna vitu vingi sana vitakavyobadilika kuanzia kwenye mtazamo wako mpaka kwenye utendaji wako wa kibiashara.

Kwa kutoshiriki semina hii ni kama umeamua kugoma kufikia mafanikio makubwa kupitia biashara yako. Yaani ni sawa na umeoneshwa njia itakayokuwezesha kufikia mafanikio lakini wewe ukasema sina haja ya kupita njia hiyo, nimesharidhika na nilipofika sasa. Sio kitu kibaya kuridhika, ila kwa ulimwengu wa sasa ambapo mambo yanabadilika kwa kasi, unajiandalia kupotea kwenye biashara.

Kwa kushiriki semina hii ni kama unapata nafasi ya kuwa na mimi kwa mwezi mzima, kuniuliza swali lolote kuhusiana na biashara yako na ukapatiwa majibu. Huwezi kuja kupata tena nafasi ya kukaa na mimi kwa mwezi mzima na kuuliza chochote unachotaka kuuliza na ukajibiwa. Huu ni muda wako wa kipekee.

Kama umewahi kukutana na mimi kwa ajili ya ushauri utakuwa unaelewa vizuri utaratibu ninaotumia. Kama hujawahi kukutana na mimi kwa ajili ya ushauri moja ya utaratibu wangu ni gharama ndogo unayotakiwa kuchangia ambayo kwa sasa ni tsh elfu 20 na tunakuwa na mazungumzo ya saa moja. Lakini kwa kupitia semina hii unalipia tsh elfu 30 kwa mwezi mzima, yaani ni sawa na tsh elfu moja kila siku. Yaani ni sawa na punguzo la asilimia 95 la gharama halisi ya kupata muda wa kukaa na mimi na tukashauriana kuhusu maendeleo ya biashara yako.

Hii sio nafasi ya wewe kukosa, labda uwe umegoma kwenda mbele zaidi. Uwe umeamua kwmaba hutaki kufikia mafanikio kwenye biashara yako na umeamua kuendelea kuwa kawaida tu.

Kwa ufupi kama hukuitia yatakayofundishwa kwenye semina hii ni haya hapa;

SEMINA YA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA.

Anza, kuza na fanikiwa kupitia biashara.

Yatakayofundishwa;

1. Utangulizi

1.1. Huu ni wakati mzuri wa wewe kuwa kwenye biashara.

1.2. Unawezakufanikiwa kwenye biashara.

1.3. Utakachokipata kwenye kozi hii.

2. Wazo la biashara

2.1. Biashara sahihi kwako kufanya

2.2. Jinsi ya kupata wazo bora la biashara

2.3. Jinsi ya kuboresha wazo lako la biashara

2.4. Baadhi ya mawazo ya biashara.

3. Mchanganuo wa biashara.

3.1. Umuhimu wa mchanganuo

3.2. Vitu muhimu vya kuweka kwenye mchanganuo wako

3.3. Udhaifu na uimara wako

3.4. Utafiti wa biashara yako

3.5. Ushindani.

3.6. Kuajiri wasaidizi bora kwenye biashara yako.

4. Mtaji na vyanzo vyake.

4.1. Aina za mtaji unaohitaji kwenye biashara

4.2. Mtaji wa fedha na vyanzo vyake

4.3. Njia bora za wewe kupata mtaji wa biashara.

5. Urasimishaji wa biashara

5.1. Umuhimu wa kusajili biashara yako.

5.2. Aina za usajili na faida zake

5.3. Hatua za kusajili biashara yako

5.4. Umuhimu na jinsi ya kulinda biashara yako.

6. Thamani ya biashara yako

6.1. Maandalizi ya bidhaa au huduma

6.2. Upatikanaji na upakiaji wa bidhaa au huduma

6.3. Upangaji wa bei.

7. Masoko na uuzaji.

7.1. Chagua soko la biashara yako

7.2. Mpango bora wa kutangaza biashara yako.

7.3. Njia rahisi za kutangaza biashara yako.

7.4. Mbinu za kuongeza mauzo kwenye biashara yako.

8. Mzunguko wa fedha.

8.1. Mauzo na faida.

8.2. Gharama muhimu za biashara

8.3. Gharama za kuepuka kwneye biashara

8.4. Kujilipa wewe mwenyewe.

8.5. Hesabu za fedha na umuhimu wa mhasibu.

9. Huduma kwa wateja.

9.1. Lengo la biashara ni kutengeneza wateja.

9.2. Jinsi ya kutoa huduma bora kwa mteja.

9.3. Mfanye mteja atangaze biashara yako.

9.4. Mteja ni mfalme na mwisho wa ufalme wake.

10. Changamoto za biashara.

10.1. Changamoto zinazoua biashara nyingi

10.2. Umuhimu wa mabadiliko

10.3. Mbinu za kufufua biashara inayokufa.

11. Mafanikio ya biashara yako

11.1. Jifunze kila siku

11.2. Matumizi mazuri ya muda

11.3. Kujihamasisha mwenyewe

11.4. Mafunzo kwa wafanyakazi wako

11.5. Usimamizi mzuri wa biashara yako.

11.6. Kununua uhuru wako kutoka kwenye biashara yako.

Leo ndio siku ya mwisho kwa wewe kupata nafasi ya kujifunz amambo yote hayo muhimu. Tuma ada ya mafunzo tsh elfu 30 kwa namba 0717396253/0755953887 na utume ujumbe wenye jina lako na email yako ili uweze kupata nafasi ya kushiriki semina hii.

KUMBUKA LEO TAREHE 01/05/2015 NDIO MWISHO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO HAYA. SIKU YA LEO IKIISHA UNAKUWA UMEIKOSA NAFASI HII YA KIPEKEE AMBAYO HAIWEZI KUTOKEA TENA.

Karibu sana kwenye semina hii.

TUPO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: