Leo ni siku ya mwisho ya kujiunga na SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA. Kwa maelezo zaidi bonyeza HAPA.
Kujifunza kila siku ndio hitaji la chini kabisa ili kuweza kufikia mafanikio kwenye maisha. Na kwenye biashara hii ni muhimu zaidi kwa sababu mabadiliko makubwa yanatokea wkenye biashara kila siku.
Kuna mbinu nyingi mpya za kukuwezesha kukuza biashara yako zinazogunduliwa kila siku. Kama utagoma kujifunza, unakuwa umejiandaa kuachwa nyuma.
Ni njia zipi ambazo wewe mfanyabiashara unaweza kuzitumia ili kujifunza kila siku?
1. Tembelea mitandao mbalimbali itakayokuwezesha wewe kujifunza. Mitandao kama AMKA MTANZANIA, KISIMA CHA MAARIFA na JIONGEZE UFAHAMU inakupatia mambo mbalimbali yatakayokuwezesha wewe kukuza biashara yako. Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA na utapata fursa kubwa ya kujifunza kuhusu biashara, tabia za mafanikio, na uongozi. Pia utapata fursa ya kukutana na wafanyabiashara wengine na kushirikia mijadala mbalimbali kwenye kundi la wasap ambayo itakuwezesha wewe kukuza biashara yako.
2. Soma vitabu. Kama hujawahi kusoma kitabu chochote cha biashara, hujui unachofanya na unajiandaa kushindwa. Hata kama muda wako ni mchache kiasi gani soma angalau kitabu kimoja cha biashara kila mwezi. Ukiweza kusoma viwili kwa mwezi au kitabu kimoja kila wiki utakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi.
SOMA; Huu Ndio Uwekezaji Bora Zaidi Unaoweza Kuufanya.
3. Hudhuria semina za biashara. Hapa utajifunza mambo mengi zaidi na kukutana an wengine pia.
4. Jifunze kutokana na uzoefu wako mwenyewe. Kama kuna makosa umewahi kufanya usiyarudie, kama kuna kitu umewahi kufanya na majibu yakawa mazuri, kitumie vizuri na boresha zaidi.
5. Jifunze kutoka wka wengine. Mazuri wanayofanya yaige na yaboreshe zaidi. Mabaya yanayowarudisha nyuma, yaepuke.
Kujifunza kila siku ni sehemu ya mafanikio yako katika biashara, usiache sehemu hii muhimu.
SOMA; Kitu Pekee Kinachoweza Kuiharibu Siku Yako Na Jinsi Unavyoweza Kuepuka…
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.