Moja ya changamoto zinazowasumbua watu wengi kwenye biashara ni kuanza upya biashara kila siku na kila mara. Hali hii imefanya biashara zionekane ni ngumu sana kuliko ugumu wenyewe.
Mtu anaanzaje biashara upya kila siku? Sio kwamba mtu anafunga biashara yake na kuanza upya, ila uendeshaji wake wa biashara unakua ni kuanza upya kila mara.
Kwa mfano biashara inapoanza kwa mara ya kwanza kuna mbinu ambazo mtu utatumia kwa mara ya kwanza kutengeneza wateja wako wa kwanza kwenye biashara. Baada ya kujua ni mbinu gani zinafaa kwenye biashara yako na zilizowez akukuletea wateja, kinachofuata ni kurudia mchakato ule uliofanya mara ya kwanza na kuendelea kuuboresha. Nguvu ya kupata mteja wa 20 kwenye biashara haiwezi kuwa kubwa kama nguvu ya kumpata mteja wa kwanza.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuibadili Dunia.
Lakini kwa wafanyabiashara wengi kadiri wanaongeza wateja ndivyo inavyozidi kuwa vigumu kwao kuwatafuta. Na hivyo kuwa kama ndio wanaanza tena biashara. Kwa nini hali hii hutokea kwa baadhi ya wafanyabiashara?
1. Hawatoi huduma bora kwa wale wateja walionao sasa na kuwafanya wateja hawa kuwa mabalozi wao wazuri. Wanatoa huduma ya kawaida au wakati mwingine ya hovyo na hivyo wateja kutokusema lolote kwa wenzao kuhusiana na biashara hiyo, au hata kulalamika kwamba sio biashara nzuri. Sasa wewe inakuwa kazi kwako kuanz akutafuta wateja wengine wapya.
2. Hawatengenezi mfumo rahisi wa kuwapata na kuwafanya wateja wabaki kwenye biashara.
SOMA; Unaweza Kwenda Umbali Mrefu Kiasi Gani?
Ni kitu gani unaweza kufanya ili kuepuka kuanz abiashara upya kila mara?
Anza kwa kujali wateja ulionao sasa, wape huduma nzuri sana ambayo hawajawahi kuipata popote na hawataweza kuipata sehemu nyingine yoyote. Wafanye wawe mashabiki wako wakubwa na wawaambie wengine wengi kuhusiana na huduma bora wanayoipata kutoka kwako. Utaona wateja wengi wanatiririka kwenye biashara yako.
Kumbuka, hili litachukua muda, endelea kuweka juhudi, endelea kufanya mabadiliko na kujaribu njia mpya. Kuna ambayo itafanya vizuri na hii itakuletea mafanikio makubwa.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.