Kanuni 6 Za Kuweza Kukusaidia Kuishi Wewe Kama Wewe Katika Maisha Yako.

Mara nyingi ni kitu ambacho nimekuwa nikikiongelea kuwa kama utaweza kuishi wewe kama wewe na kuacha tabia ya kuiga maisha ya wengine, basi kwa sehemu kubwa katika maisha yako utaweza kuishi maisha ya furaha na mafanikio makubwa sana, kwani utakuwa unafanya mambo ambayo unayapenda na itakuwa ni rahisi kwako kuweza kufanikiwa.

Kutaka kuishi kama mwingine hiyo kwako itakuwa ni sawa na kupoteza muda, kwani mara nyingi yale mambo ambayo unakuwa unaiga ni lazima utayafanya sio kwa ufanisi na furaha kubwa moyoni mwako, hivyo kwa lugha rahisi hutaweza kufanikiwa. Siri kubwa ya kuweza kubadili maisha yako ni kuweza kuishi wewe kama wewe na kufuata malengo na mipango uliyojiwekea.

ISHI WEWE

Achana na tabia hasa ile ya kufuata makundi ambayo hayawezi kukusaidia Mara nyingi wengi wanaofuata makundi huwa ni watu wa kuishia kati ama kupotea kabisa. Ili uweze kuishi wewe kama wewe ni muhimu kuzijua kanuni zitakazoweza kukusaidia kuishi wewe kama wewe na kufanikiwa kwa kiwango cha juu. Lakini je, unajua ni kanuni zipi zitakazoweza kukusaidia kuishi wewe kama wewe?

SOMA; NENO LA LEO; Umuhimu Wa Kuchepuka…

1. Weka vipaumbele katika maisha yako.

Siri kubwa inayoweza kukuwezesha kuishi wewe kama wewe ni kuweka vipaumbele katika maisha yako. Haijalishi unaishi maisha gani lakini ni muhimu kwako kuweka vipaumbele vilivyo muhimu tu na sio kufanya kila kitu. Haujaletwa duniani kufanya kila kitu. Kama ni hivyo chagua yale yalio muhimu kwako tu na kisha uyatekeleze. Kwa kuweka vipaumbele ndivyo utakavyojikuta unakuwa unaishi wewe kama wewe na kuachana na kufuata makundi ambayo yanaweza kukupoteza.

2. Weka mikakati ya kufikia malengo yako.

Ni muhimu pia kuweka mikakati ya kuweza kufikia malengo yako kama una nia ya kweli ya kuwa wewe kama wewe. Kwa kuwa na mikakati hiyo itakusaidia wewe kuwa imara na kutoweza kuyumbishwa na kitu chochote mpaka uone malengo yako yanatimia. Mara nyingi watu wengi ambao hawana mikakati mizuri ya maisha yao kwa ujumla ni watu ambao hujikuta tu ni watu wa kuyumbishwa na kufuata makundi bila hata wao kujijua.

SOMA; Kuwa Unachotaka Kuwa, Sema Unachojisikia Kusema, Kwa Sababu…

3. Chagua njia sahihi ya kukufanikisha.

Ili uweze kuwa wewe kama wewe katika maisha yako, ni muhimu kwako kuweza kuchagua njia sahihi utakayoamua kuifuata ili kufikia mafanikio hayo. Utakapokuwa umechagua njia sahihi, hiyo ina maana kuwa utakuwa umeamua kufuata malengo yako na hutaweza kuyumbishwa na kitu chochote. Kama usipojua ni kipi cha kufanya katika maisha yako itakuwa ni ngumu sana kwako kuwa wewe kama wewe, maana kila wakati utakuwa ni mtu wa kuiga tu.

4. Tambua thamani uliyonayo.

Kanuni pekee na ya muhimu itakayoweza kukuwezesha kuishi wewe kama wewe ni kutambua thamani uliyonayo katika maisha yako. Unapotambua thamani uliyonayo katika maisha yako kwanza hiyo itakusaidia kujua nini unachotakiwa kukifanya ukiwa wewe kama wewe. Wengi kwa kutokujua thamani walizonazo hujikuta ni watu wa kuiga mambo na kuamini wengine ndio bora zaidi yao. Kama unataka kuishi wewe kama wewe, tambua kwanza thamani uliyonayo.

5. Chagua vitu muhimu unavyovipenda kweli.

Wakati mwingine unaweza ukashindwa kuwa wewe kama wewe kutokana na kutokuwa na uchaguzi mzuri wa yale mambo muhimu unayoyapenda. Ni vizuri kujua yale mambo unayoyapenda na kisha uyatekeleze ama kuyafanya. Kwa kushindwa kuchagua mambo unayoyapenda kila kitu kwako utakuwa unakirukia na kukifuata na kukiona ni muhimu jambo ambalo kiuhalisia kumbe litakuwa linakutoa nje ya mstari wa kuwa wewe kama wewe.

SOMA; Kama Utazingatia Kitu Hiki katika Biashara Yako, Ni Lazima Uwe Tajiri.

6. Acha kukata tamaa.

Kati ya kitu ambacho hutakiwi kufanya katika maisha yako ni kukata tamaa wewe na kuamini huwezi tena kufanikiwa. Unapokuwa unakata tamaa hiyo inakuwa inamaanisha kuwa unakuwa umeamua kushindwa kuwa wewe kama wewe, kwani unakuwa unaamini kuwa huwezi tena kufanikiwa. Maisha yako mara nyingi yanakutaka kusimama imara kila wakati na kuamini kuwa unaweza ukashinda hata katikati ya changamoto nyingi na ndivyo hivyo unakuwa wewe kama wewe. Hujachelewa kufanya chochote unachokitaka katika maisha yako unaweza ila usipokata tamaa.

Mwisho kabisa, utaweza kuyafurahia maisha yako zaidi kama utakuwa wewe kama wewe. Ikiwa utaendelea kujaribu kuishi kama wengine hiyo itakuwa ni sawa na kupoteza muda. Kumbuka msingi mkubwa wa mafanikio upo katika wewe. Kama utakuwa unaiga tu, tayari ujue umepotea maisha yako hayatakuwa yamafanikio sana. Hizo ndizo kanuni muhimu za kukusaidia kuweza kuishi wewe kama wewe.

Kwa makala nyingine nzuri hakikisha unatembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora.

Tunakutakia kila kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,

0713 048035,

ingwangwalu@gmail.com

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: