Lengo la biashara sio kutengeneza faida. Kama utakataa sentensi hiyo na una biashara fanya jaribio. Endesha biashara yako kwa lengo moja tu, kupata faida. Na hivyo tumia njia yoyote unayoona itakuwezesha kukuletea faida. Utaipata faida hii kwa muda mfupi lakini biashara haitokua, itakufa.
Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa makala hizi za BIASHARA LEO huna haja ya kuanza kujaribu vitu ambavyo vitakuweka kwenye hatari kibiashara. Hii ni kwa sababu tayari unayo nafasi ya kujifunza mambo mengi kuhusiana na biashara na kuepuka makosa ambayo unayafanya na yanaweza kukufikisha pabaya.
SOMA; Lengo La Biashara Sio Kupata Faida, Bali Ni Hili Hapa.
Leo nataka usahau kuhusu kukuza faida na uweke mawazo yako kwneye kukuza ushawishi wa biashara yako. Wekeza kwenye kuhakikisha unatoa huduma ambazo mteja hawezi kuzipata sehemu nyingine. Hata kama unafanya biashara ya bidhaa zinazoweza kupatikana kila mahali, basi hakikisha wewe unazitoa kwa njia ya kipekee ambapo mteja atajiona ni wa pekee na hivyo kuendele akufanya biashara na wewe.
Mfanye mteja ajisikie kuw asehemu ya biashara yako, aone ni wajibu wake kukuletea wateja wengi zaidi. Na kila mteja mpya anayekuja, matarajio yake yanafikiwa kwa huduma atakayopata.
Ukifikiria kuhusu faida tu, utasahau kutoa huduma za msingi ambazo ndio zinazoleta faida. Ila unapofikiria kuhusu kutoa huduma za msingi, kuhusu kuongeza ushawishi wa biashara yako unaoa ndege wawili kw ajiwe moja. Unatengeneza wateja ambao wanakuamini na wa kudumu kwenye biashara yako na wakati huo huo unaongeza faida kwenye biashara yako.
SOMA; Sifa Sita(6) Unazohitaji Ili Kuwa Mjasiriamali Bora.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.