njia rahisi ya kupata fedha umekosea njia, hapa sikupi njia rahisi ya kupata
fedha, haipo, kwa sababu kama ingekuwepo na jinsi ambavyo watu wanaipenda fedha
kila mtu asingeijua.
Hapa nataka nikushirikishe njia rahisi ya wewe kufikia uhuru wa
kifedha. Unakuwa na uhuru wa kifedha pale ambapo fedha sio changamoto kwenye
maisha yako. Yaani una uhuru wa kipato ambacho kinaingia bila ya wewe kufanya
kazi moja kwa moja na unaweza kupata mahitaji yako yote bila ya kuwa na
changamoto kubwa.
SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki
Kimoja.
Leo nataka nikuambie kwmaba uhuru wa kifedha hautegemei kiasi
kuwa na kiasi kikubwa cha fedha, ila kuweza kutumia vizuri kiasi cha fedha
ulichonacho hata kama ni kidogo.
Leo fanya zoezi hili moja, fikiria ungekuwa na dola bilioni moja
kwenye akaunti zako za benki(hii ni sawa na trilioni mbili za kitanzania) ni
mambo gani ungefanya. Yaani fikiria fedha sio tatizo, unazo zakukutosha na hata
usipofanya kazi bado utakula wewe, watoto wako na wajukuu zako. Je ni vitu gani
ambavyo ungefanya?
Orodhesha vitu hivi kwenye karatasi, usiache hata kimoja.
Chochote unachofikiria utafanya kiorodheshe. Baada ya kukamilisha hatua hii ya
kuorodhesha sasa nenda kwenye hatua ya pili na muhimu zaidi.
Hatua ya pili; kwenye orodha yako ondoa vitu vyote ambavyo ni
vya anasa. Vifute kabisa vitu vyote ambavyo ni vya anasa, ambavyo sio muhimu uwe
navyo ndio maisha yaende. Kwa mfano kama uliorodhesha kuwa na nyumba tatu za
kuishi, huwezi kuishi kwenye nyumba tatu kwa wakati mmoja.
Hatua ya tatu ni kuanza sasa kufanya yale ambayo yamebaki kwenye
orodha yako baada ya kuondoa yale ambayo ni anasa.
Kwa kufanya hivi utafikia uhuru wa kifedha kwa sababu; hutakuwa
na matumizi makubwa, utafanya vitu ambavyo unavipenda na hutojali sana kuhusu
fedha.
TAMKO LA LEO;
Najua uhuru wa kifedha unapatikana pale ambapo ninafanya kitu
ninachopenda kufanya na kuwa na matumizi mazuri ya fedha zangu. Kama ningekuwa
na fedha za kutosha ningependelea kufanya vitu vifuatavyo, na vitu hivi ndio
nitaanz akuvifanya sasa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 148 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita
Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na
maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza
hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.