Kama Ni Ubaya Huwa Unautengeneza Hivi…Katika Maisha Yako.

Nakumbuka kuna siku nilinunua gazeti, nikiwa natarajia kupata taarifa nzuri za kunipa moyo zaidi, za kunifanya nione kwamba, dunia ni mahala salama. Nilianza kulisoma gazeti lile na kukutana na vichwa vya habari kama hivi: Mtu mmoja kajiua! Wanawake wanne wamenajisiwa! Matukio 20 ya wizi yameripotiwa! Watu 100 wamekufa katika mlipuko!

Matukio yote hayo yalikuwa yameandikwa katika ukurasa mmoja tu. Baada ya kuona hivyo, nilipata uvivu wa kuendelea kulisoma gazeti lile! Niliogopa kwamba, huenda kila ukurasa ungekuwa na taarifa zenye ukakasi kama zile. Sikuwa nataka kuiharibu siku yangu!

Halafu siku hiyohiyo jioni, ile nafungua runinga tu, nikakutana na habari za vurugu na picha zake. Nilijifunza kwamba, taarifa za vurugu na uharibifu siyo kitu cha kukifurahia, labda kama umelazimika kwa sababu fulani fulani kufanya hivyo. Niliona kwa hali hiyo, sina haja ya kutazama runinga. Niliamua kufanya kazi zangu zingine.

Mara nyingi tupo salama pale kunapokuwa hakuna tatizo lolote duniani. Hatuwezi kuikimbia jamii tulimokulia. Hakuna mtu annayependa kuwa muuaji hivihivi tu. mazingira humlazimisha mtu kuweza kufanya vitendo. Leo tunasimulia waliofanya unyama. Kesho itakuwa zamu yako kufanyiwa unyama huo, kwani wahenga walisema mwenzio akinyolewa wewe tia maji.


Iko siku tutaumizwa na simba tuliyeamua kumfuga sisi wenyewe! Sasa tunatakiwa kuamua ama kuusimamisha uhalifu huu duniani au kuacha uendelee. Au unataka kuchukua hatua pale yatakapokufika? Uchaguzi pia ni wetu.

Nasema mazingira nikiwa na maana kuwa, muuaji, mteketazaji, mharifu, ni lazima awe amekerwa au kufundishwa kabla kwamba, hayo ndiyo maisha. Mtu hauwi kwa sababu amezaliwa ili kuuwa, hapana.

Ndiyo maana kama hutaki kuwa na wauaji jiulize ni kwa kiwango gani, umezuia jambo hilo kupitia fikra, kauli, vitendo na hisia zako?

Kwa mujibu wa Waldo Emerson, ubaya huwa tunajifunza kutoka kwenye jamii zetu kwani kila binadamu alizaliwa akiwa roho nyeupe. Kama dunia ingekuwa chanya nasi tungekuwa chanya. Dunia si chanya ndiyo maana wengi waliomo si chanya! Dhamira yetu ya ukatili imetudhibiti kabisa. Hata tukijificha vipi iko siku tabia hii mbaya  itajidhihirisha katika jamii. Na ndiyo hizi vurugu tunazoziona kwenye magazeti na kwenye runinga.

Binadamu anaweza kuwa mgonjwa ama kimwili au kiakili. Ugonjwa wa akili humfanya mtu kufanya mambo ya ajabu. Mgonjwa wa akili anaweza kufanya chochote kile.

Anaweza kufanya kitu cha hatari ama kisicho cha hatari. Kila mmmoja wetu anatakiwa kujipa wasaa wa kufikiri. Wapi tunakoelekea? tunataka maisha gani ya baadae? Tunajali tunapomuona mwenzetu ameauawa? Inakuaje Yule aiyeuliwa anapokuwa mtu karibu na wewe? Lazima utalia!

Suala hapa siyo kuwaheshimu wauaji, au wale wanaonajisi. Wala siyo kuwapa matumaini wahenga . Katika jamii jamii ya waungwana , kama walifu na wote wasio wahalifu ni wahanga kama kila mmoja weti anataka kuwa muungwana sasa, wahalifu hatari wa namna hii wanatoka wapi? Jibu ni rahisi tu katika jamii zetu. Kama hujui ubaya na matatizo yote huwa yanatengenezwa hapa tu, kwenye jamii unayoishi.


Unapompiga myonge unajitakia kuwa mhanga wake pale atakapoamua  kukugeukia wewe. Dunia yetu imeharibika sasa kwa sababu tunatumia nguvu zetu vibaya. Badala ya kutumia nguvu zetu kuweza kutufanikisha tunazitumia katika mambo ambayo hayafai kama uhalifu tunaouona mara kwa mara kupiti vyombo vya habari.

Kitu cha msingi kuliko vyote ambaho binadamu anatakiwa kukifafanya katika dunia ya sasa ni kuihifadhi dunia ili iweze kuwa sehemu ya amani ambayo itakuwezesha kutafuta mafanikio kwa urahisi. Roho ya upendo inatakiwa  iwe ndiyo lengo letu. Hatupaswi kuwa kama wanyama.

Kwa kufanya hivyo tutaweza kusambaza wema dunia kwa kutumia nguvu za mapokezano na mwisho wa siku tutajikuta tupo katika dunia yenye usalama. Hakikisha unakuwa mwadilifu kwa maisha yako na ya wengine, acha kuwaumiza wengine na pia hakikisha hujiumizi wewe mwenyewe.

Tuakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea AMKA MATANZANIA  kujifunza kila siku.

IMANI NGWANGWALU,
0713 048035,

2 thoughts on “Kama Ni Ubaya Huwa Unautengeneza Hivi…Katika Maisha Yako.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: