Kama biashara haina soko kuna jambo moja tuna uhakika nalo, itakufa. Hakuna biashara ambayo itaweza kujiendesha bila ya kuwa na wateja. Mafanikio yako wewe kama mfanyabiashara ni kiasi gani cha soko umeshika.

Kuna biashara nyingi sana ambazo zinakufa kwa kukosa soko. Leo nataka nikupe sababu moja kwa nini biashara yako haina soko na ni kitu gani unaweza kufanya ili kuiokoa biashara yako.

Sababu moja kubwa biashara zinakosa soko ni pale mfanyabiashara anapokuja na suluhisho halafu akaanza kutafuta tatizo. Yaani wewe una suluhisho la tatizo ambalo watu hawalijui bado. Katika hali kama hii utakuwa na wakati mgumu sana wa kuwa na soko la biashara yako. Utahitaji kuanza kuwapa watu elimu kwanza ndio waweze kununua bidhaa au huduma yako. Hii ni kazi kubwa sana kwa mfanyabiashara ambaye anaanza.

SOMA; Kila Mtu Anawinda Kitu Hiki Muhimu Ulichonacho, Kuwa Makini.

Badala ya kuja na suluhisho ndio utafute soko, hebu angalia tatizo linalowasumbua watu wengi na litafutie suluhisho. Ukishakuja na suluhisho utaona watu wengi wanalikimbilia, na kama wakipata majibu mazuri watawaambia wengine na wengine na wengine.

Usifanye kosa la kutengeneza suluhisho kabla ya kuwepo kwa tatizo, angalia tatizo linalowasumbua wengi na tengeneza suluhisho, utakuwa na biashara yenye mafanikio.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.