Unafanyia kazi haya unayojifunza kwenye kipengele hiki cha BIASHARA LEO? Kama unafanyia tushirikishe kwenye maoni hapo chini ni jinsi gani biashara yako inabadilika. Na kama hufanyii kazi tuambie ni kwa nini? Yote tunayojifunza kwenye kipengele hiki sio vitu vya kufurahia kusoma, bali ni vitu unatakiwa kufanya. Unasoma kitu hapa na unakifanyia kazi, kikishindwa unajifunza na kikifanikiwa unajifunza pia.
Leo nakupa njia tatu muhimu za kukuza biashara yako. Zisome hapa na zifanyie kazi, iwe ni njia moja au njia zote. Najua kila mtu anataka biashara yake ikue, sasa kwa nini usifanyie kazi?
Njia ya kwanza; kupata wateja wapya.
Mpaka sasa unawajua ni watu gani ambao ni wateja wako. Kukuza biashara yako angalia njia za kupata wateja wapya na wapate.
Njia ya pili; ongeza kiasi cha fedha mteja anakupatia.
Kwa wateja wale ambao tayari unao kwenye biashara yako, ongeza kiasi cha fedha ambacho mteja anakupatia. Najua nikisema hivi mara moja unafikiria kuongeza bei. Ni moja ya njia za kuongeza kisi cha fedha, ila njia nyingine nzuri ni kumfanya mteja anunue zaidi, au kumpatia mahitaji mengine ambayo angekwenda kununua sehemu nyingine.
Njia ya tatu; ongeza muda ambao mteja anafanya biashara na wewe.
Kila mteja ana muda wake kwenye biashara yako. Kulingana na biashara yako ilivyo, mteja anaweza kuwa anakaa na wewe miezi kadhaa au hata mwaka au miaka kadhaa. Kadiri mteja anavyoendelea kufanya biashara na wewe, ndivyo unavyoendelea kukuza biashara yako. Angalia ni jinsi gani unaweza kuwafanya wateja wako waendelee kufanya biashara na wewe kwa muda mrefu.
SOMA; USHAURI; Una Mtaji Lakini Hujui Ni Biashara Gani Ufanye? Soma Hapa Kujua.
Fanyia kazi mambo haya matatu. Ongeza wateja wapya, ongeza kiasi cha fedha mteja anakupatia na ongeza muda unaofanya biashara na mteja. Mambo haya yatakuza biashara yako na kukuleta faida zaidi na kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.